Kwa miaka mingi kumekuwa na utata na usiri mkubwa kuhusu kutua ya ndege aina ya BA 149 huko Kuwait wakati wa Uvamizi wa Iraqi uliofanyika mwaka 1990 kukiwa na madai kwamba Serikali ya Uingereza iliitumia ndege hiyo kwa kuendesha shughuli maalumu za siri na kusababisha abiria na wafanyakazi wa ndege waliokuwemo kuteswa kwa miezi mitano.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Uingereza iliondoka London jioni ya Agosti 1, 1990 na kwa safari ya Asia kupitia Kuwait, usiku wa siku hiyo uvamizi wa Iraq ulifanyika. Ilitua asubuhi ya Agosti 2, ikiwa ni ndege pekee kutua muda huo huku ndege zingine zikihairisha na kuta katika viwanja vingine.
Anthony Paice alipelekwa Kuwait mwaka 1988, kwa amajukumu aliyoyaita ni ya kijajusi kwenye siasa, ingawa awali alitajwa kama afisa maalumu (M16) akifaya kazi maalumu katika Ubalozi wa Uingereza nchini Kuwait.
Anasema hakuwa anaweza kupinga zinazoitwa 'tuhuma za uongo' kwa sababu ya kubanwa na sheria lakini sasa anasema anataka kuweka hadharani akishirikiana na wale walioteswa na na kuathirika na tukio hilo.
"Nina uhakika kabisa kwamba kulikua na shughuli za kijasusi za kijeshi zilizofanywa kupitia ndege hiyo ya BA 149 licha ya maafisa kunaka jambo hilo mara kwa mara," alisema Paice.
Ameiambia BBC kwamba, anaamini kwamba kulikuwa na jaribio la haraka lililoandaliwa kijajuzi' lililoendeshwa na vikosi maalumu vya jeshi, jaribio ambalo yeye na hata balozi hawakuwa wanafahamu.
"Hatukujua lolote," akisema ni jaribio lililokusudiwa kabisa na ambalo 'linakanushwa kwa makusudi'. Kuna tuhuma kwamba Bwana Paice alihusika kwenye operesheni hiyo au alipotosha kuhusu kama ndege hiyo ingeweza kutua Kuwait ama la. Anasema tuhuma hizo ni za uzushi.
Abiria waliotekwa walitumika kama ngao dhidi ya mashambulizi
Bwana Paice anasema alizungumza na mwakilishi wa ndege hiyo jioni ya Agosti 1 kuhusu kuanza kwa mzozo kati ya Kuwait na Iraq, lakini ilikuwa kabla ya uvamizi kuanza.
"Kama una ndege inakatiza hapa usiku wa manane, inaweza kupita," anakumbuka Paice.
Lakini alionya kwamba uvamizi ama shambulio lolote Kuwait linaweza kufanyika asububi na kwamba dege hiyo isingeweza kutua asubuhi iliyofuata.
Clive Earthy, Aliyekuwa kiongozi wa huduma za ndege hiyo, anakumbuka kwamba, kulikuwa na raia mmoja wa Uingereza aliyevalia sare za jeshi na walisalimiana mlangoni punde baada ya ndege hiyo kutua Kuwait.
Mtu huyo alimwambia kwamba amekuja kuonana na watu 10 waliopanda ndege hiyo kutoka uwanja wa Heathrow, London. Walivyojitokeza watu hao 10, walitokomea na hawakuonekana tena.
"Watu hao walipewa kipaumbele cha kwanza kutoka na kuingia Kuwait, na abiria wangu,wake kwa waume, na watoto, walifuata" Bwana Earthy aliiambia BBC.
Anasema anaona Serikali ya Uingereza inawajibika kwa kile kilichofuata baada ya abiria na wahudumu wa ndege walitekwa na kushikiliwa na vikosi vya Iraqi.
Baadhi wengine wangeliachiliwa, lakini baadhi waliteswa, wapo walionyanyaswa kingono na wengine kushindishwa njaa. Wengi walitumika na Iraqi kama ngao ya kibinadamu ili kuzuia kushambuliwa na mabomu na vikosi vya magharibi. Mateka hao walikuja kuachiliwa baada ya miezi mitano.
Je ni watu gani wa ajabu na wasiofahamika walikuwa kwenye ndege hiyo?
Stephen Davis, mwandishi wa kitabu kipya kinachoitwa 'Operation Trojan Horse', anasema aliwahoji baadhi ya watu hao kwa kificho na wate waliohusika kwenye mpango huyo. Anaamini mpango huo ulihusisha kupelekea timu maalumu ya kuendesha shughuli za kijasusi na kupelekea mrejesho .
Anaamini pia Mamlaka za Uingereza hazikutarajia kwamba uwanja wa ndege uliotumika ungevamiwa na vikosi vya Iraqi kwa haraka kama ulivyotokea. Badala yake walitarajia kwamba watu hao wangeweza kushuka mapema na ndege ingeendelea na safari zake.
Anasema nauli za watu hao zililipwa kupitia akaunti ya Jeshi, hivyo shirika la ndege la Uingereza lilikuwa linafahamu kuhusu Mpango huo.
Ikijibu tuhuma hizo, Waziri wa ulinzi alirejelea taarifa zilizopita kwenye bunge, akisema : "Mwaka 2007, Serikali ya Uingereza inalithibitishia Bunge kwamba mwaka 1990 serikali haikuitumia ndege hiyo kwa namna yoyote kwa shughuli za kijeshi."
Shirika lenyewe la ndege pia lilikataa kusema chochote, likirejelea kwenye taarifa za serikali za kukana kuhusika kwake.
Wito wa kuomba radhi.
Jinny Gill kijana mwenye umri wa miaka 18, alikuwa amekaa kwenye viti vya mwisho mwisho vya ndege hiyo, akiwa na dada yake. Anawakumbuka watu wawili waliokuwa wamekaa karibu nay eye, anasema hakuna hata mmoja aliyezungumza neon hata moja kwenye safari nzima.
Anaamini kwamba walikuwa sehemu ya vikosi maalumu.
Ndege ilipotua , anaeleza kwamba hakukua na wafanyakazi wa uwanja wandege waliokuwepo uwanjani wala ndege yoyote zaidi ya ndege ya shirika la ndege la Kuwait.
Anasema yeye na dada yake walishuka na kutembea hatua chache uwanjani hapo kwa lengo la kunyosha mwili, kabla ya kuona mlipuko mkubwa kwenye uwanja huo.
"Hapo ndipo tulipogundua kuwa mambo hayako sawa," sAliiambia BBC. "Hatukujua wapi pa kukimbia na nini cha kufanya." Anasema hakuwaona wale watu wawili waliokuwa wamekaa nae. "Nilitaka ukweli uwekwe wazi, pude tu baada ya kurudi Uingereza, lakini hakuna lolote mpaka leo," alisema.
Kitabu cha Davis kilizinduliwa kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini London, ikiadhimishwa miaka 31 tangu kutokea kwa tukio hilo, huku kitabu hicho kikiwahusisha pia baadhi ya watu waliotekwa. Huku Bwa Paice akizungumzia hilo kwa mara ya kwanza.

