Virusi vya corona: Kampuni ya Ndege ya Tanzania, ATCL yarejesha safari zake kwenda India

 


tz

Kampuni ya ndege ya Tanzania (ATCL) imerudisha safari zake za kwenda India kuanzia Jumapili Agosti 29, 2021.

Msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa amesema serikali inajipanga kufungua maeneo mengine ingawa safari za Nairobi nchini Kenya zitaanza muda wowote hivi karibuni.

Aidha kwenye upande wa vipimo vya Covid 19, gharama imepungua kutoka na kwa nchi za jirani vipimo vimekuwa bure, gazeti la Mwananchi limeandika

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilisitisha safari zake za ndege kati ya Dar as Salaam na Mumbai (India ) kuanzia tarehe 4 mwezi Mei na ilihaidi kutoa taarifa nyingine ya kurudisha safari hizo.

Hatua hiyo ya kusitisha safari za India ni kutokana na kuwepo kwa ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 .

India ilikuwa inakabiliwa na janga kubwa la virusi vya corona.

Hospitali zilikuwa zimelemewa wagonjwa wengi na ripoti za watu kufariki mitaani .

Malawi ilipiga marufuku pia wasafiri wanaotoka India, pamoja na Bangladesh, Brazil na Pakistan kutokana kusambaa kwa virusi vya corona katika mataifa hayo.

Maelezo ya video,

Virusi vya corona: 'Hatuna nafasi ya kuichoma miili'

Nchi nyingine zilizositisha safari za kwenda na kutoka India

kenya

Si Tanzania pekee kwa upande wa Afrika Mashariki iliyositisha safari za ndege kwenda nchini India.

Kenya imesitisha kwa muda safari za ndege za abiria wanaotoka India. Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ongezeko la maambukizi ya Corona nchini India .

Uganda nayo ilipiga marufuku safari zote za ndege kutoka India kuanzia tarehe 1 mwezi Mei ili kuzuia wimbi jingine la janga la corona nchini humo .

Waziri wa Afya nchini humo Ruth Aceng alisema serikali ilichukua hatua mbalimbali ili kuzuia kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya virusi hivyo .

Hata hivyo kuna safari kutoka India ambazo Uganda ilisema hazitaathiriwa na marufuku hiyo na ni pamoja na ;Safari za ndege za mizigo ambazo wahudumu wake hawataruhisiwa kutoka kwneye ndege zao

Kusimama kwa muda wa safari za ndege ambapo abiria hawashuki.

Ndege ambazo zitapatawa na hali ya dharura.

Operesheni zinazohusiana na misaada ya kibinadamu ,misaada ya matibabu na huduma za uokoaji zilizoidhinishwa na mamlaka husika.

Raia wa Uganda wanaorejea nyumbani kutoka India kwa matibabu.

Nchi nyingine zilizopiga marufuku safari za ndege India ni pamoja na Canada, falme za kiarabu na Uingereza -marufuku zilizoanza kutekelezwa jumamosi iliyopita lakini hazitathiri ndege za kubeba mizigo.

ug

Hatua za tahadhari

Siku ya jumatatu Serikali ya Tanzania ilitoa muongozo mpya kuhusu ugonjwa wa corona ambapo wasafiri watakaokuwa wanatoka katika nchi zenye maambukizo ya virusi vipya vya corona watatakiwa kukaa karantini kwa siku 14.

Muongozo huo uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya nchi hiyo Profesa Abel Makubi ulianza kufanya kazi Mei 4 2021, unaeleza kuwa karantini hiyo itawahusu wasafiri ambao ni wakaazi na wageni.

Kabla ya kwenda karantini kwanza watafanyiwa vipimo vya lazima vya corona.

Kwa wageni watatakiwa kukaa karantini kwa gharama zao "watachagua eneo moja katika orodha itakayotolewa na serikali."

Wasafiri ambao ni wakaazi wa Tanzania wataruhiswa kujitenga kwa siku 14 katika nyumba zao wenyewe.

Mwezi mei mwaka jana Tanzania iliondoa karantini ya lazima kwa wasafiri kutaka nje ya nchi hiyo na badala yake wakatangaza kuwa kutafanyika vipimo vya ugonjwa huo.

Wizara ya Afya ya Tanzania imeeleza kuwa nchi hizo zenye virusi vipya vya corona zitatambuliwa kupitia taarifa zinazotolewa kila siku na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Kwa sasa virusi vipya vinavyogonga vichwa vya habari zaidi ni vya India na Brazil.

Wataalamu wanatahadharisha kuwa idadi ya maambukizi inaweza ikawa kubwa zaidi ya hiyo

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post