Wanafunzi watano wafa ajalini wakiwa wamepanda ‘mshikaki’

0

 

shikakipic

Baadhi ya miili ya wanafunzi watano walikufa baada ya pikipiki waliokuwa wamepanda kugongwa na fuso

Chalinze.  Wanafunzi watano wa Shule ya Sekondari Kimange wilayani hapa Mkoa wa Pwani wamefariki dunia baada ya pikipiki waliokuwa wamepanda kwa mtindo wa ‘mshikaki’ kugongwa na gari aina ya fuso.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Pwani, Abubakar Kunenge  amesema  kuwa wanafunzi wanne walifariki dunia papo hapo jana usiku baada ya fuso lililokuwa linatokea Arusha kwenda Dar es Salaam kuwagonga, huku mmoja akipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Jeshi Kihangaiko.

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete amewataja wanafunzi hao waliofariki ni  Laya Ubwa  Masudi (16),  Furaha Athumani (16) na Athumani Mchafu (17) wote wa kidato cha tatu.

Wengine ni  Athumani Bushiri (15)  na Amina Msomba (15) waliokuwa wanasoma kidato cha kwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigeza amesema:"Ni kweli kuna wanafunzi wamefariki dunia na wote watano walikuwa wamepakizana kwenye pilipiki hiyo moja  na walikuwa wamemaliza michezo yao ya kishule kwenye shule jirani ya Kwamakocho wakawa wanarudi makwao."

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa fuso na mwendo kasi kwa kushindwa kumudu gari hilo.

Wanafunzi hao wamezikwa leo Agosti 7, 2021.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable