YANGA YATUPWA NJE KAGAME CUP 2021,YACHAPWA 3-1 NA EXPRESS YA UGANDA

0

 

Timu ya Yanga imeshindwa kutinga nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Kagame, baada kufungwa mabao 3-1 na Express ya Uganda mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mabao ya Express yalifungwa na  Godfrey dk 14, Muzamiru dk 35 na Kambale dk 52 na bao pekee la Yanga limefungwa na Paul Godfrey dk 71 kwa shuti kali akiwa nje ya 18.

Kwa ushindi huo Express imeongoza kundi na Nafasi ya pili kushikwa na  Big Bullets kutoka Malawi ambayo imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidhi ya Atlabara FC kutoka Sudan Kusin.

Michuano hiyo itaendelea majira ya saa moja usiku mechi za Kundi B,vinara wa kundi hilo Azam FC watashuka dimbani kucheza na KMKM ya Zanzibar na KCCA FC ya Uganda itacheza na Le Messager Ngozi ya Burundi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable