
Chanzo cha picha, Reuters
Marekani itaondoa vikwazo vya usafiri ilivyoweka kwa mataifa manane ya kusini mwa Afrika kutokana aina mpya ya virusi vya corona,omicron.
Ikulu ya White House ilisema hatua hiyo ya tarehe 29 Novemba, inayoathiri Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji, Namibia, Lesotho, Eswatini na Malawi, itaondolewa kufikia mkesha wa mwaka mpya.
Afisa huyo alisema vikwazo havikuwa muhimu tena huku kukiwa na mlipuko wa kesi za Omicron. Nchini Marekani .
Aina hiyo sasa inaunda zaidi ya kesi zote mpya za Marekani.
"Vizuizi vilitupa muda wa kuelewa Omicron na tunajua chanjo zetu zilizopo zinafanya kazi dhidi ya Omicron," aliandika katika twitter katibu msaidizi wa habari wa White House Kevin Munoz.
Vizuizi viliwekwa kwanza na EU na Uingereza. Marekani na mataifa mengine mengi yalifuata mkondo huo.
Hatua hiyo ilikosolewa vikali, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiiita "ubaguzi wa kusafiri".
Akithibitisha hatua hiyo, mshauri mkuu wa Ikulu ya White House, Dk Anthony Fauci, alisema mapema mwezi huu "ilifanyika wakati tulikuwa gizani" kuhusu Omicron.
"Sote tunasikia vibaya sana kuhusu ugumu wa maisha ambao unaweza kuwekwa sio tu kwa Afrika Kusini, lakini nchi nyingine za Afrika," alisema.
Wiki iliyopita, Canada iliondoa marufuku yake yenyewe kwa wasafiri wa kigeni kutoka nchi 10 za Afrika. Afisa mmoja alisema ongezeko la kesi za Omicron za nyumbani inamaanisha masharti hayo "hayahitajiki tena".
Vyombo vya habari vya Canada hapo awali viliripoti kwamba marufuku hiyo iliwalazimu baadhi ya raia kusafiri kupitia Ethiopia walipokuwa wakirejea nyumbani licha ya ushauri dhidi ya kutembelea taifa hilo la Pembe ya Afrika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Katika wiki za hivi karibuni Marekani imeimarisha zaidi mahitaji yake ya vipimo. Wasafiri wote wa kimataifa lazima watoe uthibitisho wa matokeo hasi ndani ya siku moja ya safari yao ya ndege, bila kujali hali ya chanjo.
Rais Joe Biden - ambaye ameitaja Omicron "sababu ya wasiwasi, sio sababu ya hofu" - hadi sasa amekataa kuunga mkono hatua za kuweka marufuku za kutoka nje zinazoonekana katika baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya.
Marufuku hiyo haikuwazuia Wamarekani kurejea nchini kutoka eneo hilo na iliwahusu tu raia wasio Wamarekani.
Madaktari nchini Afrika Kusini - ambapo Omicron iliripotiwa mara ya kwanza - walisema mapema kwamba maambukizi kutoka kwa aina hiyo mpya ya virusi yalikuwa yanasababisha tu ugonjwa mdogo. Matokeo haya yameungwa mkono na utafiti nchini Uingereza.
Aina hii imeenea kwa kasi zaidi kuliko aina yoyote ya awali nchini Marekani lakini bado haijasababisha ongezeko kubwa la watu kulazwa hospitalini.
Ni kifo kimoja tu cha Marekani hadi sasa ambacho kimehusishwa na Omicron: mwanamume wa Texas mwenye umri wa miaka 50 ambaye hakuchanjwa na alikuwa na maradhi nyemelezi