Manchester United wamekubaliana mpango ambao utamfanya mshambuliaji wake Anthony martial kujiunga na Sevilla kwa mkopo kwa kipindi chote kilichosalia cha msimu , iwapo atapita vipimo vya matibabu.
Makubaliano hayo hayaipatii Sevilla uwezo wa kumnunua mchezaji huyo, isipokuwa klabu hiyo ya Uhispania itaweza kumlipa mshahara wake.
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 , amekuwa akilengwa na klabu hiyo kwa miezi kadhaa sasa.
Martial ambaye alijiunga kutoka Monaco kwa dau la £36m 2015, has ameambia kocha Ralf Rangnick anataka kuondoka .
Mkufunzi wa Aston Villa na nahodha wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard anavutiwa na mlinzi wa Reds na England Joe Gomez, 24. (Football Insider)
Wakati huo huo, United imeongeza kasi ya kutafuta kocha mpya, huku kocha mkuu wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino, kocha wa Ajax Erik ten Hag, mkufunzi wa Uhispania Luis Enrique na Julen Lopetegui wa Sevilla wakizingatiwa. (Athletic - subscription required)
Manchester United walikuwa miongoni mwa vilabu vilivyomchunguza winga wa Colombia Luis Diaz akiichezea Porto mwishoni mwa juma. Atletico Madrid na Borussia Dortmund pia wanamfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye amefunga mabao 14 katika mechi 18 za Primeira Liga msimu huu. (O Jogo - in Portuguese)
Newcastle wanavutiwa na mshambuliaji wa Manchester United, Muingereza Jesse Lingard, 29, na kiungo wa kati wa Brighton raia wa Mali Yves Bissouma, 25. (Mirror)
Nice pia anashawishika kutaka kumnunua Lingard, ambaye anahusishwa pia na West Ham. (Foot Mercato - in French)
Manchester City na Liverpool wamefanya mazungumzo kuhusu kumsajili winga wa Uholanzi Cody Gakpo mwenye umri wa miaka 22 kutoka PSV Eindhoven.(Voetbal International - in Dutch)
Mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 21, ameiambia Fiorentina kuwa anataka kujiunga na wapinzani katika ligi ya Serie A, Juventus.(90 Min)
The Gunners, hata hivyo, italazimika kutimiza masharti ya pauni milioni 70 ikiwa wanataka kumsajili Isak kabla ya tarehe ya mwisho ya kuhama Jumatatu ijayo. (Express)
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ni shabiki mkubwa wa Calvert-Lewin lakini jaribio lolote la kumsajili halitafanyika hadi msimu wa joto.(Star)
Aubameyang ameweka wazi kuwa hana nia ya kuhamia Saudi Arabia ambako amekuwa akihusishwa na klabu mbili. (Star)
Tottenham wana uhakika wa kukamilisha usajili wa pauni milioni 20 wa winga wa Wolves kutoka Uhispania Adama Traore, 25. Wolves wanataka pauni milioni 25 kwa ajili ya mchezaji huyo ambaye mkataba wake unamalizika msimu wa joto wa 2023. (Sky Sports)
Wakati huo huo, Spurs wameanzisha mazungumzo na klabu ya Ufaransa ya Angers juu ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 mwenye umri wa miaka 18 Mohamed-Ali Cho, ambaye klabu zake za zamani ni Everton na Paris St-Germain. (Football Insider)
Bayern Munich imefanya mawasiliano na wakala wa kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 24, katika nia ya kuzishinda Chelsea, Manchester City na Paris St-Germain ili kuinasa saini yake. (Marca)
Borussia Dortmund have opened talks with Red Bull Salzburg over a possible 40 million euro (£33.5m) deal for 20-year-old Germany forward Karim Adeyemi. (Sky Sport - in German






