ICJ yaiagiza Uganda kuilipa DRC $325m kwa uvamizi iliyofanya kati ya 1998 na 2003

0


 

Uganda iIishirikiana na wanamgambo wa ndani kupora dhahabu kutoka kwa Ituri

Uganda imeagizwa kulipa $325m (£240m) kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa jukumu lake katika mzozo nchini humo.

Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) iliamua Uganda ilikuwa imekiuka kanuni za kimataifa kama jeshi linaloikalia kimabavu kati ya 1998 na 2003.

Majaji waligundua kuwa Uganda ilihusika na vifo vya watu 10-15,000 katika eneo la Ituri mashariki.

Wanajeshi wa Uganda pia walipatikana na hatia ya kupora dhahabu, almasi na mbao.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilidai dola bilioni 11 lakini majaji walitupilia mbali sehemu kadhaa za madai hayo na kuamua kiwango cha chini zaidi.

ICJ iliamuru Uganda kulipa awamu tano za kila mwaka za $65m kati ya 2022 na 2026, na awamu ya kwanza italipwa mnamo Septemba.

Uganda ilikuwa imesema kuwa mabilioni ya yanayodaiwa na DR Congo yangeharibu uchumi wake. Mahakama ilisema amri yake itakuwa "ndani ya uwezo wa Uganda kulipa".

Gharama ya $325m inashughulikia:

• $225m kwa fidia kwa watu

• $40m kwa uharibifu wa mali

• $60m kwa rasilimali zilizoporwa

Katika hukumu yake, mahakama ilisema: "Malipo yaliyotolewa kwa DRC kwa uharibifu wa watu na mali yanaonyesha madhara waliyopata watu binafsi na jamii kutokana na Uganda kukiuka majukumu yake ya kimataifa."

DR Congo ilifungua kesi dhidi ya Uganda mwaka 1999 kwa vitendo vya uchokozi wa kutumia silaha dhidi yake na raia wake. Ilishutumu wanajeshi wa Uganda kwa uporaji na ukiukaji wa haki za binadamu.

Makundi mengi yenye silaha yamekuwa yakisababisha uharibifu mkubwa wa madini mashariki mwa DR Congo kwa miongo kadhaa.

Katika miaka ya 1990, wanajeshi kutoka Uganda na Rwanda mara mbili walivamia taifa hilo jirani, wakifanya kazi na wanamgambo wa ndani kuiangusha serikali.

Waliteta kuwa waliingilia kati kuzuia mzozo wa DR Congo usisambae katika mipaka yao.

Uamuzi wa mahakama ni wa mwisho na hakuna njia ya kukata rufaa, lakini mahakama ya dunia haina njia ya kutekeleza uamuzi wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable