KAKA WA DIAMOND,RICARDO MOMO NA MKEWE BADO WAPOWAPO SANA
Siku kadhaa kupita kumekuwa na maneno mengi sana yakielekezwa kwa kaka wa Msanii Diamond ajulikanaye kama Ricardo Momo ]Mzee wa Kudere] ambapo wambea walikuwa wakidai kuwa wameachana na mkewe Malaika na hiyo ni baada ya watu kutokuwaona karibu kama ilivyo zamani ambapo ilikuwa unapomkuta Momo basi lazima umkute na mkewe Malaika
Hatimae mke huyo ameamua kuwaziba midomo wambea kwa kupost video akiwa na mumewe huyo wakiwa na mtoto wao ambapo inaelezwa kuwa wapo pamoja sehemu za kula raha kusherehekea siku ya kuzaliwa Ricardo Momo
Mbali na hivyo lakini pia mwanamama huyo ameamua kujibu komenti kwenye moja ya kurasa za udaku ambao ulipost video hiyo na kuuliza kumbe wamerudiana na ndipo mwana mama huyo akamjibu
"Kwani tuliachana?


Kwa mastory yote ya town like page yetu Facebook na kutufollow Instagram Msasa Online hakika hutopitwa na chochote saa 24.
#MsasaKisasaZaidi
