Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 07.02.2022: Rice, Azpilicueta, Christensen, Isak, Botman, Tevez

0


 

Kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice, 23, atakuwa anawaniwa kwenye mchakato wa uhamisho wa majira ya joto na Manchester United na Chelsea. (Sky Sports)

Barcelona wanatumai kuhitimisha uhamisho wa mlinzi wa Chelsea na Uhispania Cesar Azpilicueta, 32, na mlinzi wa kati wa Denmark Andreas Christensen, 25, baada ya siku chache.(Express)


 

Manchester United wameungana na Arsenal kumtaka mshambuliaji wa Real Sociedad Alexander Isak, 22, huku klabu hiyo ya Old Trafford ikimtazama mshambuliaji huyo wa Sweden kama mbadala wa Cristiano Ronaldo.(Football London)

Rais wa Lille Olivier Letang anasema mlinzi wa Uholanzi Sven Botman mwenye umri wa miaka 22 - ambaye alihusishwa na kuhamia Newcastle mwezi Januari - anastahili kuchezea klabu ambayo inaweza kushinda Ligi ya Mabingwa. (Le Parisien via Fabrizio Romano)

 

Wawakilishi wa mshambuliaji wa zamani wa West Ham, Manchester United na Manchester City Carlos Tevez wako kwenye mazungumzo na DC United inayoshiriki ligi ya MLS. Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 38 amekuwa mchezaji huru tangu alipoondoka Boca Juniors Julai mwaka jana. (The Athletic via Mail)

Manchester United wamekubali ada ya pauni milioni 12 na Flamengo kwa ajili ya Andreas Pereira, klabu ya nyumbani kwao ambapo Mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 26 yuko kwa mkopo. (Mirror)


 

Mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Kevin Phillips anasema Liverpool inaweza kusajili mrithi wa muda mrefu wa Mohamed Salah wa Misri, 29, mshambuliaji wa Arsenal na Uingereza Bukayo Saka, 20. (Football Insider)

Mlinzi wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, 28, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, anataka pauni 225,000 kwa wiki kusalia Stamford Bridge, huku The Blues wakitoa ofa ya pauni 140,000 kwa wiki. (Mirror)


 th

Mkurugenzi wa RB Leipzig Oliver Mintzlaff ana imani kiungo wa kati Mfaransa Christopher Nkunku, 24, atasalia katika klabu hiyo licha ya kutakiwa na Liverpool na Arsenal. (Sky 90)

Beki wa Ufaransa Layvin Kurzawa, 29, alitolewa kwa mkopo kwa Lille na Paris St-Germain katika dirisha la uhamisho la Januari. (Le Parisien, in French)

Kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Gavi, 17, amekataa kuongezewa mkataba kwa kuwa mshahara haukidhi matakwa yake. (Sport, in Spanish)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable