Watu 12 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na vipande vilivyoanguka hii leo baada ya jeshi nchini Saudi Arabia kuilipua ndege isiyotumia rubani ya waasi ya Yemen iliyokuwa ikilenga uwanja wa ndege ulioko karibu na mpaka.
Kulingana na maafisa vipande hivyo vilianguka baada ya ndege hiyo kudunguliwa kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abha, ambao awali ulilengwa katika shambulizi kama hilo na waasi wa Houthi.
Maafisa wa shirika la habari la Saudi Arabia wamesema kupitia Twitter kwamba watachukua hatua kali ili kujibu kitisho hicho dhidi ya viwanja vya ndege na wasafiri. Kulingana na shirika hilo raia 12 wa mataifa mbalimbali walijeruhiwa baada ya ndege hiyo kudunguliwa.