OSE MUHANDO AMPA POLE PROFESA JAY,AMWAMBIA KUUGUA NI IBADA....
Muimbaji wa nyimbo za Injili Rose Muhando ameungana na Watanzania wengi kwenye kumpa pole Msanii Profesa Jay ambaye inaelezwa amelazwa kwa siku kadhaa sasa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na maradhi ndipo msanii huyo akaona atumie ukurasa wake wa Instagram kumpa pole msanii mwenzake huyo ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Mikumi kwa tiketi ya CHADEMA.
Ameandika Rose Muhando
'Magonjwa sio mpango wa Mungu bali ni hila za shetani ndio maana hata Ayubu alijaribiwa na shetani kupitia magonjwa na kwasababu sisi ni Binadamu kuugua ni ibada, inatukumbusha kwamba Mungu yupo na tunapaswa kumshukuru kwa kuendelea kutupa uhai kila iitwayo leo, hali unayoipitia niliwahi ipitia miaka miwili iliyopita lakini kwa sababu namuamini sana Mungu niliivuka, nakuombea sana @professorjaytz Mungu wetu ni waupendo na kwakua tunamwamini basi utapona.''
Kwa habari kemkem za kuhabarisha kuelimisha na kuburudisha
