AMSHITAKI MKEWE KWA MADAI YA KAMZALIA WATOTO WENYE SURA MBAYA KULIPWA TSH. MILIONI 279 FIDIA.....

0

 



Kwa mujibu wa ripoti ya tovuti mbalimbali huko nchink China kuna kisa cha kushangaza kiliocha watu kwenye sintofahamu baada ya mwanaume mmoja aitwaye Jian Feng, kumshitaki mkewe kwa kumzalia watoto wenye sura mbaya.
Feng anasema alimuoa mkewe kwa furaha na upendo, lakini furaha hiyo imetoweka na kuwasababishia mfarakano wa kindoa baada ya mkewe huyo kumzalia watoto wenye sura mbaya kiasi hata cha kuwaogopa.
Kwa kujitazama utanashati wake, pamoja na urembo wa mkewe, bwana Feng hakuamini kama watoto wale wangekuwa ni wa kwake, hivyo alimshutumu mkewe kwa kukosa uaminifu katika ndoa. Lakini hata hivyo, vipimo vya DNA vilithibitisha kuwa watoto wale ni wa kwake.
Kwa bahati, baadaye mke wa Feng, alikuja kukiri wazi na kuthibitisha kwamba, huko nyuma kabla hawajafunga ndoa, alipata kutumia kiasi cha dola $100,000 (€77,000) kufanyiwa upasuaji nchini Korea Kusini wa kujibadili mwonekano wake (Cosmetic surgery).
Kufuatia kukiri huko, Feng alimshitaki mkewe kwa kosa la kugushi mwonekano, na kutosema kweli juu ya upasuaji aliofanya kiasi cha kupelekea aonekane mrembo kinyume na uhalisia. Jaji alikubaliana na malalamiko ya Feng, na kumtaka mke alipe fidia ya dola $120,000 (€102900) sawa na zaidi ya Tsh. Milioni 279.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable