MESSI,MODRIC KARATA YA MWISHO

0

 #MCIHEZO Washindi wawili wa Ballon d'Or wanaovaa jezi namba 10, ambao wote walishafika fainali ya kombe la dunia kwa nyakati tofauti lakini wakashindwa kutwaa taji hilo. Manahodha wawili wa timu za taifa za Argentina na Croatia Lionel Messi la Pulga na Luka Modric leo mmoja wapo atakuwa na nafasi ya mwisho kufikia kilele cha soka lake kujaribu kutwaa kombe la Dunia. 



Messi ana umri wa miaka 35 na Luka Modric ana umri wa miaka 37 mmoja leo atafuzu kucheza mchezo wa fainali na mwingine atasubiri kucheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu na huenda maisha yao ya Kombe la Dunia wawili hao yakaishia hapo. 


Argentina itawakabili Croatia saa 4:00 usiku wa leo katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar.


#FIFAWorldCup #Qatar2022 #Croatia #Argentina #Messi #Modric #WorldCup2022 #EastAfricaRadio

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable