Baada ya ukimya wa zaidi ya mwaka mmoja na nusu, hatimaye mwimbaji wa Bongofleva, Aslay amewapa mashabiki wake muziki wake kile walichokosa kwa muda mrefu kwa kuachia ngoma mbili, 'Mozzah' na 'Follow Me' akimshirkisha Harmonize.
Hata hivyo, ujio huu ni darasa kwa wasanii na mashabiki kuhusu starehe, matumizi ya fedha, nidhamu ya kazi, umilivu na kukubali kuanza upya.
Aslay alikuwa miongoni mwa wasanii wanne waliounda kundi la Yamoto Band lilovunjika rasmi mwishoni mwa mwaka 2016, wengine ni Mbosso, Enock Bella na Beka Flavour.
Baada ya kuachana na Yamoto Band, Aslay aliweza kutoa nyimbo 15 ndani ya miezi 11 (Aprili 10, 2017 hadi Februari 22, 2018) na kupata mapokezi makubwa.
Ujio wake huu mpya, ni baada ya kusaini kufanya kazi na Menejimenti ya RockStar Africa na Lebo ya Sony Music Entertainment Africa, akiwa ameungana na Ommy Dimpoz, Abigail Chams na Young Lunya kwa hapa Tanzania.
Aslay alikuwa kimya tangu alipoachia wimbo wake 'Nashangaa' hapo Januari 2021, na tangu kabla ya hapo hakuwa na wakati mzuri wa kuachia ngoma kama ambavyo mashabiki wake walikuwa wamemzoea.
"Nilidanganywa sana, niliibiwa sana, karibia nipoteze maisha yangu kwa msongo wa mawazo kwa kunywa pombe, na msongo wa kumkumbuka mama yangu, lakini yote ni ustaa na nilichagua mwenyewe maisha ya kuwa staa" Aslay akieleza sababu za ukimya wake.
"Sasa hivi nimekua, akili yangu imekua na nina uzoefu wa yote niliyopitia, sasa ni kufanya kazi na kuangalia maisha mengine mapya" anasema Aslay katika dokumentari yake, Mimi ni Bongo Fleva.
Inaendelea....!
cc @aslayisihaka
#avmediainfos #breaknews #radio #vpl #epl #tmz #netflix #tv #youtube #habari #bongofleva #bongomovie #muziki #movie #Tanzania #Kenya #uganda #burundi #rwanda