Emoji na Maana Zake! #Emoji

0

Emoji zimepata umaarufu sana kwa miaka kadhaa sasa kama sehemu muhimu ya mawasiliano. Leo tunakuletea orodha ya emoji na maana zake.



Emoji ni picha au nembo inayopachikwa katika maandishi na kutumika katika jumbe za kielektroniki pamoja na kurasa za tovuti. Kuna aina mbalimbali za emoji kama emoji za sura, vitu vya kawaida, maeneo, aina za hali ya hewa na wanyama.

Neno Emoji limetoka kwenye lugha ya kijapan na maana yake ni picha. Emoji zilianza kutumika katika simu za wajapan mwaka 1997 na kupata umaarufu zaidi mwaka 2010 zilipoanza kutumiwa na kampuni za watengeneza simu. Kuna zaidi ya Emoji 3000 zinazotumika mpaka sasa. Emoji hutumiwa na watu kujieleza, kukuza mwingiliano katika maongezi na kuonyesha hisia kwa njia ya ujumbe.

Orodha ya Emoji na maana zake.

  • 😀 Uso wa Kutabasamu
  • 😃 Uso wa Kutabasamu na wenye macho makubwa
  • 😄 Uso wa kutabasamu/kucheka na macho yakiwa yamefungwa
  • 😁 Tabasamu lenye kicheko
  • 😆 Kicheko kikubwa cha furaha
  • 😅 Kicheko kikubwa hadi jasho
  • 🤣 Kicheko cha hadi kujigaragaza
  • 😂 Kicheko kinacholeta machozi ya furaha
  • 🙂 Tabasamu kidogo
  • 🙃 Kichwa juu chini
  • 😉 Kukonyeza
  • 😊 Tabasamu lililo jaa furaha tele
  • 😇 Tabasamu lenye urembo wa upindo juu
  • 🥰 Tabasamu lililojaa upendo
  • 😍 Tabasamu la kimahaba
  • 🤩 Tabasamu la kushangilia mambo mazuri
  • 😘 Busu linalotuma upendo
  • 😗 Uso unaobusu
  • ☺️ Sura ya Tabasamu
  • 😚 Kubusu huku macho yamefungwa
  • 😙 Kubusu huku macho yanafuraha
  • 🥲 Uso unaotabasamu na chozi la furaha
  • 😋 Uso wenye matamanio ya msosi
  • 😛 Kutoa ulimi nje
  • 😜 Kukonyeza huku ulimi uko nje
  • 🤪 Uso wa mchezo/Kuonesha ukichaa
  • 😝 Uso wa Kiutani na Ulimi Nje
  • 🤑 Uso wa Unaonesha ‘PESA PESA’
  • 🤗 Kumbatio
  • 🤭 Mkono ukifunika mdomo / Kuishiwa maneno ya kuongea / kuchagua kukaa kimya
  • 🤫 Uso unaomnyamazisha mtu / Kaa Kimya
  • 🤔 Kuwa katika mawazo
  • 🤐 Kufunga mdomo ‘zipu’ / Siri ipo salama
  • 🤨 Kutoamini unachosikia au Kuona / Kushangazwa
  • 😐 Sura isiyo onesha hisia
  • 😑 Sura isiyo na hisia
  • 😶 Uso bila mdomo
  • 😏 Uso wa tabasamu la kiutani
  • 😒 Uso wa Kutopendezwa na Mambo
  • 🙄 Uso ukiwa na macho yanayotazama juu / Maringo
  • 😬 Grimacing Face – Hii ni emoji ambayo inaleta mchanganyiko sana kwani inatokea tofauti sana kwenye huduma au simu tofauti. Hapa chini ndivyo inavyotokea kwenye huduma mbalimbali.
  • Emoji na Maana Zake
    Ugumu wa emoji ni kwamba inatokea tofauti kwenye huduma na simu tofauti. Kuna wanaona ni kisura kinachofurahia jambo..na kwa wengine kinatokea kama kisuru chenye jambo tata.
    • 🤥  Sura ya kusema uongo
    • 😌  Uso wa furaha baada ya jambo au kitu
    • 😔  Uso wenye mawazo
    • 😪  Kuwa na usingizi
    • 🤤  Kuwa na tamaa ya kitu/jambo/mtu
    • 😴  Kuwa na Usingizi
    • 😷  Uso uliovaa barakoa
    • 🤒  Kipima joto mdomoni / Kujisikia kuumwa au homa
    • 🤕  Kufungwa bandeji kichwani
    • 🤢  Kujisikia kizunguzungu
    • 🤮   Kutapika
    • 🤧   Kupenga makamasi
    • 🥵   Kuhisi Joto kali
    • 🥶  Kuhisi baridi
    • 🥴 Sura ya kuchanganyikiwa
    • 😵 Sura ya kizunguzungu
    • 🤯 Mpasuko/Mlipuko wa kichwa
    • 🤠 Kichwa kilichovaa kofia za ‘Cowboy’
    • 🥳 Kusheherekea
    • 🥸  Kutopendezwa na jambo
    • 😎 Sura yenye miwani na yenye tabasamu
    • 🤓 Sura ya ujuaji
    • 🧐 Sura yenye miwani jicho moja
    • 😕 Sura ya kutoelewa
    • 😟 Sura ya wasiwasi
    • 🙁 Sura iliyokunjamana kidogo
    • ☹️ Sura iliyokunjamana
    • 😮 Sura yenye mdomo wazi
    • 😯 Sura iliyotulia
    • 😲 Sura ya mshangao
    • 😳 Sura ya Kushtuka
    • 🥺 Sura ya kusihi
    • 😦 Sura iliyokunjamana na yenye mdomo wazi
    • 😧 Sura yenye uchungu
    • 😨 Sura ya woga
    • 😰 Sura ya woga yenye majasho
    • 😥 Sura ya huzuni
    • 😢 Sura ya kulia
    • 😭 Sura ya kulia
    • 😱 Uso Unaopiga Mayowe Kwa Hofu
    • 😖 Sura ya kuchukizwa
    • 😣 Sura ya kuchukizwa
    • 😞 Sura ya kukata tamaa
    • 😓 Sura ya kuchoka na majasho
    • 😩 Sura ya kulalamika
    • 😫 Sura ya kuchoka
    • 🥱 Sura ya kupiga miayo
    • 😤 Sura ya kuchukia
    • 😡 Sura ya kukasirika
    • 😠 Sura ya kukasirika
    • 🤬 Sura yenye alama kwenye mdomo
    • 😈 Sura yenye tabasam na mapembe
    • 👿 Sura yenye hasira na pembe
    • 💀 Fuvu la kichwa
    • ☠️ Fuvu na mifupa
    • 💩 Kinyesi
    • 🤡 Mchekeshaji
    • 👹 Zimwi
    • 👺 Goblini
    • 👻 Roho
    • 👽 Mgeni kutoka sayari nyingine
    • 🤖 Roboti
    • 😺 Paka anayecheka
    • 😸 Paka anayecheka kwa furaha
    • 😹 Paka mwenye machozi ya furaha
    • 😻 Paka mwenye kopa machoni
    • 😼 Paka mwenye tabasam
    • 😽 Paka anayebusu
    • 🙀 Paka aliyechoka
    • 😿 Paka anayelia
    • 😾 Paka aliyenuna
    • 💋 Alama ya kubusu
    • 👋 Kupunga Mkono
    • 🤚 Kunyoosha mkono
    • 🖐️ Mkono wenye vidole vilivyosambazwa
    • ✋ Mkono ulionyooshwa
    • 🖖 Saluti ya kivulcani
    • 👌  Sawa
    • 🤏 Kubana Mkono
    • ✌️  Mkono wa ushindi
    • 🤞 Kukunja vidole
    • 🤟 Ishara ya Nakupenda
    • 🤘  Alama ya mapembe
    • 🤙 Nipigie
    • 👈 Mkono kuonyesha mbele
    • 👉 Mkono kuonyesha nyuma
    • 👆 Mkono kuonyesha juu
    • 🖕 Kidole cha kati
    • 👇 Mkono kuonyesha chini
    • ☝️ Kidole kuonyesha juu
    • 👍 Kidole gumba
    • 👎 Kidole gumba chini
    • ✊ Ngumi Iliyoinuliwa
    • 👊 Ngumi inayokujia
    • 🤛 Ngumi kuelekea kushoto
    • 🤜 Ngumi kuelekea kulia
    • 👏 Kupiga makofi
    • 🙌 Kuinua mikono
    • 👐 Kufungua mikono
    • 🤲 Viganja juu
    • 🤝 Kupeana mkono
    • 🙏 Mikono kugusana
    • ✍️ Mkono unaoandika
    • 💅 Kupaka rangi kucha
    • 🤳 Kujipiga Selfie
    • 💪 Kutunisha misuli
    • 🦾 Mkono wa chuma
    • 🦿 Mguu wa chuma
    • 🦵 Mguu
    • 🦶 Unyayo
    • 👂 Skio
    • 🦻 Skio lenye kifaa cha kusikilizia
    • 👃 Pua
    • 🧠 Ubongo
    • 🫁 Mapafu
    • 🦷 Jino
    • 🦴 Mfupa
    • 👀 Macho
    • 👁️ Jicho
    • 👅 Ulimi
    • 👄 Mdomo
    • 👶 Mtoto
    • 👦 Mtoto wa kiume
    • 👧 Mtoto wa kike
    • 🧑 Mtu
    • 👨 Mwanaume
    • 🧔 Mwanaume mwenye ndevu
    • 👨‍🦰  Mwanamke 
    • 👨‍🦳 Mwanaume mwenye nywele nyeupe
    • 👨‍🦲 Mwanaume mwenye kipara
    • 👩 Mwanamke
    • 👩‍🦰  Mwanamke mwenye nyewele nyekundu
    • 👩‍🦳 Mwanamke mwenye nywele nyeupe
    • 👩‍🦲  Mwanamke mwenye kipara
    • 🧓  Mzee
    • 🙍 Mtu kukunja uso
    • 🙍‍♂️ Mwanaume kukunja uso
    • 🙍‍♀️ Mwanamke kukunja uso
    • 🙅 Mtu kuashiria hapana
    • 🙅‍♂️ Mwanaume kuashiria hapana
    • 🙅‍♀️ Mwanamke kuashiria hapana
    • 🙆 Mtu kuashiria ndio
    • 🙆‍♂️ Mwanaume kuashiria ndio
    • 🙆‍♀️ Mwanamke kuashiria ndio
    • 🙋‍♂️ Mwanaume kunyoosha mkono
    • 🙋‍♀️ Mwanamke kunyoosha mkono
    • 🧏‍♂️ Kiziwi wa kiume
    • 🧏‍♀️ Kiziwi wa kike
    • 🙇 Mtu kuinama
    • 🙇‍♂️ Mwanaume kuinama
    • 🙇‍♀️ Mwanamke kuinama
    • 🤦 Mtu akiziba uso
    • 🤦‍♂️ Mwanaume akiziba uso
    • 🤦‍♀️ Mwanamke akiziba uso
    • 🤷‍♂️ Mwanume akiinua mabega
    • 🤷‍♀️ Mwanamke akiinua mabega
    • 👨‍⚕️  Mtaalamu wa afya wakiume
    • 👩‍⚕️  Mtaalamu wa afya wakike
    • 👨‍🎓 Mwanafunzi wakiume
    • 👩‍🎓 Mwanafunzi wakike
    • 👨‍🏫 Mwalimu wakike
    • 👨‍⚖️ Jaji wakiume
    • 👩‍⚖️ Jaji wakike
    • 👨‍🌾 Mkulima wakiume
    • 👩‍🌾 Mkulima wakike
    • 👨‍🍳 Mpishi wakiume
    • 👩‍🍳 Mpishi wakike
    • 👨‍🔧 Fundi wakiume
    • 👩‍🔧 Fundi wakike
    • 👨‍🏭 Mfanyakazi wa kiwandani wakiume
    • 👩‍🏭 Mfanyakazi wa kiwandani wakike
    • 👨‍💼  Mfanyakazi wa ofisini wakiume
    • 👩‍💼 Mfanyakazi wa ofisini wakike
    • 👨‍🔬 Mwanasayansi wakiume
    • 👩‍🔬 Mwanasayansi wakike
    • 👨‍💻 Mtaalamu wa teknolojia wakiume
    • 👩‍💻 Mtaalamu wa teknolojia wakike
    • 👨‍🎤 Mwimbaji wakiume
    • 👩‍🎤 Mwimbaji wakike
    • 👨‍🎨 Mchoraji wakiume
    • 👩‍🎨 Mchoraji wakike
    • 👨‍✈️  Rubani wakiume
    • 👩‍✈️  Rubani wakike
    • 👨‍🚒 Zimamoto wakiume
    • 👩‍🚒 Zimamoto wakike
    • 👮‍♂️ Polisi wakiume
    • 👮‍♀️ Polisi wakike
    • 🕵️‍♂️ Mpelelezi wakiume
    • 🕵️‍♀️ Mpelelezi wakike
    • 💂‍♂️ Mlinzi wakiume
    • 💂‍♀️ Mlinzi wakike
    • 🥷 Ninja
    • 👷‍♂️ Fundi ujenzi wakiume
    • 👷‍♀️ Fundi ujenzi wakike
    • 🤵‍♂️ Mwanaume aliyevaa Tuxedo
    • 🤵‍♀️ Mwanamke aliyevaa in Tuxedo
    • 🤰 Mwanamke mwenye mimba
    • 🤱 Kunyonyesha
    • 👩‍🍼 Mwanamke kumpa mtoto maziwa
    • 👨‍🍼 Mwanume kumpa mtoto maziwa
    • 👼 Malaika mtoto
    • 🎅 Santa Claus
    • 🦸‍♂️ Shujaa mkuu wakiume
    • 🦸‍♀️ Shujaa mkuu wakike
    • 🦹‍♂️  Adui mkuu wakiume
    • 🦹‍♀️   Adui mkuu wakike
    • 🧙‍♂️ Mchawi wakiume
    • 🧙‍♀️ Mchawi wakike
    • 🧛‍♂️ Vampaya wakiume
    • 🧛‍♀️  Vampire wakike
    • 🧜‍♀️ Nguva
    • 🧞‍♂️  Jini la kiume
    • 🧞‍♀️ Jini la kike
    • 🧟‍♂️ Zombi wakiume
    • 🧟‍♀️ Zombi wakike
    • 🚶‍♂️ Mwanaume anayetembea
    • 🚶‍♀️ Mwanamke anayetembea
    • 🧍‍♂️ Mwanaume aliyesimama
    • 🧍‍♀️ Mwanamke aliyesimama
    • 🧎‍♂️ Mwanaume akipiga magoti
    • 🧎‍♀️ Mwanamke akipiga magoti
    • 👨‍🦽 Mlemavu wakiume
    • 👩‍🦽 Mlemavu wakike
    • 🏃‍♂️ Mwanaume akikimbia
    • 🏃‍♀️ Mwanamke akikimbia
    • 💃 Mwanamke akicheza
    • 🕺  Mwanaume akicheza
    • 🧑‍🤝‍🧑 Watu wakishikana mikono
    • 👩‍❤️‍💋‍👨 Kubusu
    • 👩‍❤️‍👨 Wapenzi
    • 👨‍👦  Familia: Baba na mtoto wakiume
    • 👨‍👦‍👦 Familia: Baba na watoto wakiume
    • 👨‍👧 Familia: Baba na mtoto wakike
    • 👨‍👧‍👦 Familia: Baba na mtoto wa kike na wa kiume
    • 👨‍👧‍👧 Familia: Baba na watoto wakike
    • 👩‍👦   Familia: Mama na mtoto wakiume
    • 👩‍👦‍👦 Familia: Mama na watoto wakiume
    • 👩‍👧  Familia: Mama na mtoto wakike
    • 👩‍👧‍👦 Familia: Mama na mtoto wa kiume na wakike
    • 👩‍👧‍👧 Familia: Mama na watoto wakike
    • 🗣️  Mtu anayeongea
    • 👣 Alama za miguu
    • 🧳 Mzigo
    • 🌂 Mwamvuli uliofungwa
    • ☂️ Mwamvuli
    • 🧵 Uzi
    • 👓 Miwani
    • 🕶️ Miwani ya jua
    • 🥽 Miwani
    • 🥼 Koti la maabara
    • 🦺 Kizibao cha usalama
    • 👔 Tai
    • 👕 Tisheti
    • 👖 Jinzi
    • 🧤 Glovzi
    • 🧥 Koti
    • 🧦 Soksi
    • 👗 Gauni
    • 👘 Kimono
    • 🥻 Sari
    • 🩱 Nguo za kuogelea
    • 🩲 Boksa
    • 🩳 Bukta
    • 👙 Bikini
    • 👚 Nguo za kike
    • 👛 Pochi
    • 👜 Pochi ya mkononi
    • 🎒 Begi
    • 👞 Viatu vya mwanaume
    • 👟 Viatu vya mazoezi
    • 🥿 Viatu vya chini
    • 👠Viatu vya juu
    • 👡 Sendo za mwanamke
    • 🩰 Viatu vya balleti
    • 👢 Buti la mwanamke
    • 👑 Krawni
    • 👒 Kofia ya mwanamke
    • 🎩 Top Hat
    • 🎓 Kofia ya mahafali
    • 🪖  Kofia ya kivita
    • ⛑️ Kofia za waokoaji
    • 💄 Lipustiki
    • 💍 Pete
    • 💼 Mkoba
    • 🩸 Tone la damu
    • Endelea kutembelea tovuti yetu uweze kujifunza mambo mbalimbali kuhusu teknolojia

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable