Mwimbaji wa Muziki wa Tanzania, Mbosso Khan amenusurika katika ajali mbaya ya barabarani

0

 Mwimbaji wa Muziki wa Tanzania, Mbosso Khan amenusurika katika ajali mbaya ya barabarani akiwa nchini Marekani.



Msanii huyo wa WCB ambaye kwa sasa yuko kwenye ziara ya kutangaza albamu yake ya Definition of Love aliyoiachia mwaka jana 2022.


Habari zinasema kwamba Mbosso Khan amepata majeraha kwenye bega lake la mkono wa kulia na mbavu za mkono wa kushoto.


Sehemu za video alizopost kwenye Instastory na mwimbaji huyo zinaonyesha kuwa gari lao lilipata mikwaruzo na gari lingine lililokuwa likienda kasi na hivyo kupata majeraha.


Polisi walifika eneo la tukio, Mbosso na wafanyakazi wake wakipatiwa matibabu ya dharura na gari la wagonjwa lililokuwa limeambatana na polisi.


Mbosso amewahakikishia mashabiki wake kuwa yuko sawa kwa ujumla licha ya kupata majeraha kwenye ajali hiyo. Bado haijafahamika iwapo Mbosso ataendelea na ziara yake kama ilivyopangwa au ajali hiyo itaathiri ratiba yake.


Nyota huyo tayari alikuwa ametumbuiza huko Phoenix Arizona na Seattle, Washington na idadi kubwa ya mashabiki walijitokeza.


#KitengeUpdates

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable