Barcelona wanakaribia kufikia mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, lakini uhamisho wa bure wa kiungo huyo aliye na umri wa miaka 32- utategemea ikiwa klabu hiyo ya Nou Camp itafanikiwa kumshawishi mshambuliaji mwenzake wa Argetina Lionel Messi, 33, kusalia nao. (AS)
Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer huenda akawauza wachezaji Jesse Lingard, 28, Juan Mata,32, Diogo Dalot 21 na Phil Jones, 29, kuongezea bajeti yake ya £80m msimu wa joto. (Metro)
Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc, amesema klabu hiyo imepatia kipaumbele kushinda Ligi ya Mabingwa kupitia Bundesliga wanapojitahidi kusalia na mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, kwa "muda mrefu iwezekanavyo". (Welt an Sonntag, via Goal)
Manchester City wamewasiliana na Sporting Lisbon kumhusu mlinzi wao Nuno Mendes wanapojiandaa kuitangulia Real Madrid katika juhudi za kumsajili nyota huyo Mreno aliye na umri wa miaka 18. (AS, via Mail)
Arsenal wanamtaka mlinzi wa Eintracht Frankfurt Mfaransa Evan N'Dicka, 21, na wameomba kupewa maelezo kuhusu hali ya kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma,24. (Express)
Chelsea inahitaji angalau euro milioni 20 kumpata mlinzi wa Italia Emerson Palmieri,26, lakini Inter Milan na Napoli pia zinataka kumsajili. (Calciomercato, via Football Italia)
Kocha wa Juventus Andrea Pirlo amesema ni "kawaida kuwepo kwa uvumi" wa hatma ya mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo katika klabu hiyo baada ya kutoka kwenye Ligi ya Mabingwa lakini mchezaji huyo, 36, "amekuwa na mchezo mzuri" kwa timu hiyo ya Serie A. (Football Italia)
