Jeshi la Polisi Mjini Magharibi Zanzibar linamshikilia Mwanaume mmoja kwa tuhuma za kutaka kusababisha kifo cha Mke wake wa pili ambae amemuoa sio chini ya wiki mbili zilizopita.
Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi Alhaji Juma Awadh amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema "Kijana anaitwa Yusufu Maulid Mussa (24) Mkazi wa Kwarara amemjeruhi Mke wake Asha Hassan Haji (28) Mkazi wa Kwarara pia na kumsababishia majeraha makubwa shingoni, Mwanamke amewaisha Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu"
"Mtuhumiwa tumeshamkamata yuko Mahabusu Kituo cha Mazizini kwa hatua zaidi, chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi.... taarifa nilizozipata hii ndoa bado ni changa sana nimeambiwa ni wiki mbili zilizopita wamefunga ndoa sasa nadhani Mapenzi yalikua bado motomoto na wivu sasa umepelekea hivyo" ——— RPC Alhaj Juma Awadh. #MillardAyoUPDATES
