Marehemu Kanali Fabian Massawe ataagwa Jumapili ya March 14 2021 Jijini Dar es salaam kwenye Kanisa la Boko Mtakatifu Isidore Bakanja na kuzikwa Jumatatu ya tarehe 15 March 2021 Kibosho Umbwe Mkoani Kilimanjaro.
Fabian Massawe ambae alifariki jana March 10 2021 Hospitalini Jijini Dar es salaam amewahi kuwa Mkuu wa Shule ya Jitegemee Dar es salaam kuanzia mwaka 1986 hadi 2002 lakini pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya za Kinondoni, Karagwe na Muleba na baadae kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera mwaka 2011.
Massawe atakumbukwa kwa mengi ikiwemo kujitoa kwake kusaidia Watu mbalimbali bila kuangalia sura, vipato vyao au wanatokea familia gani na alifurahi sana na kupambania Vijana mbalimbali kuwa na nidhamu ya maisha na kupata elimu nzuri kwa namna yoyote ile na mmoja wa Vijana waliofaidika na juhudi na ukarimu wake ni mimi Millard mwaka 2003 Dar es salaam. #RIPMzeewangu #TutaonanaBaadae
#
