Polisi kwenye Mkoa wa Pwani wamethibitisha kumkamata Mtu mmoja Raia wa Tanzania akiwa na line nyingi za simu za mkononi ambapo kati line zote 74 zilizokamatwa, line 56 ni mpya na 18 zimetoka kufanya utapeli zikiwa zimesajiliwa kwa jina moja la Moses Cosmas, jumla ya Watuhumiwa waliokamatwa kwa makosa mbalimbali ni 123.
"Huyu Moses Cosmas ana line za simu 18 ambazo zote hizo amesajili kwa jina moja na amekua akitumia kufanya utapeli, hebu fikiria kuna Mtanzania ana line 18 ambazo amesajili kwa jina moja Moses Cosmas na anatumia kitambulisho kimoja cha NIDA, huu ni uhalifu mkubwa... anaweza kutumia line hii akakutukana, akatumia nyingine akakutapeli n.k" ——— RPC Pwani Wankyo Nyigesa
