Kutana na Ernest Nkwocha, Kijana wa Nigeria ambaye amejizolea umaarufu kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutengeneza sanamu za Binadamu na Wanyama kwa kutumia matairi mabovu ya magari.
Hamasa yake ya kufanya ubunifu huu ilisukumbwa na hamu yake ya kutaka kuona Jiji la Lagos likiwa safi kwa kuondoa matairi yaliyotumika mitaani na sasa ndoto zake mpya ni kuufanya ubunifu huo ufike kwa Watu wengi Duniani.
