UTUMWA WA NGONO NI NINI?

0
UTUMWA WA NGONO:




WATU wengi ni watumwa wa ngono bila wenyewe kujua. Lakini ubongo una kazi gani katika utumwa wa ngono? Ni njia gani zilizopo katika kupambana na uraibu na kurejea katika hali ya kawaida pamoja na kujizatiti na kujihakikishia tena kuwa na maisha ya mapenzi yaliyo bora? Kitu kilicho bora, ninaamini ni kwenda hatua kwa hatua katika kulielezea tatizo hili.
Utumwa wa Ngono ni nini?








Mapenzi ya kushurutishwa, yale ya lazima, ambayo mtu analazimika kufanya bila kufuata taratibu, yaani ile tabia ya kutaka kufanya mapenzi au vitendo vya ngono kila wakati, kila mahali na mtu yeyote, ni uraibu na utumwa, tena ni tatizo ambalo linaweza kudhibitiwa. Kwa maana nyingine uraibu wa ngono ni ile tabia ya mtu kupenda kufanya mapenzi kila wakati, kila mahali, na kutotosheka na mapenzi ayapatayo.
Watu wa aina hii wako wengi, wengine hupendelea vitu fulani katika kukidhi kiu zao za mapenzi, kama vile kupiga punyeto (kujichua: kwa mwanamke na mwanaume na kuna wanawake ambao siku hizi wanapenda sana kutumia viungo bandia vya kiume ili kukidhi kiu zao, hasa wasagaji), kutazama picha za ngono, kuchungulia watu wakifanya mapenzi na mambo mengine kadha wa kadha.
Wapo pia watu; wanawake kwa wanaume, ambao hata kama wako na wapenzi wao huwa hawafikii mshindo mpaka ama wakumbuke picha ya ngono waliyopata kuiona au wamfikirie mtu ambaye wanampenda sana na wangetamani kufanya naye mapenzi.
Watu kama hawa, bila kuvuta hisia kama hizi katu hawawezi kuridhika, na mara baada ya kufikia mshindo huwa hawawezi kabisa kuendelea kufanya mapenzi kwa ngwe nyingine na hujiona kama wanajilazimisha tu!
Mapenzi bora na yanayonoga ni yale yenye mvuto na hisia. Haya hutoa nafasi ya kufurahia uhusiano ulio bora zaidi na wenye mvuto yakini. Lakini kwa baadhi ya watu, kuna msukumo wa lazima ambao huwalazimu kujiingiza katika vitendo vya ngono vilivyokithiri na visivyofaa.
Utumwa wa ngono huharibu maisha ya kawaida ya mapenzi ya mhusika. Watu walioraibiwa na ngono hawawezi kudhibiti au kuahirisha hisia zao za ngono pamoja na matendo yao. Wataendelea na vitendo vyao viuvo vya ngono, wakihangaika kuzifurahisha hisia zao za mapenzi kwa gharama yoyote ile, wengine kama siyo kujichua, huishia h...

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable