Summary
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa (Tumaini), fani ya uandishi wa habari mwaka wa pili, Prudence Patrick (21) amefikishwa kakika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa akituhumiwa kumuua mpenzi wake kwa kumnyonga hadi kufaIringa. Aliyekuwa Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa (Tumaini), fani ya uandishi wa habari mwaka wa pili, Prudence Patrick (21) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa akituhumiwa kumuua mpenzi wake kwa kumnyonga hadi kufa.Mwanafunzi huyo alifikishwa katika mahakama hiyo June 9 akituhumiwa kumuua Petronila Mwanisawa (22) kwa wivu wa mapenzi.
Prudence alisomewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi, Emmy Nsangalufu na kisha kurudishwa rumande hadi Juni 23. Katika kesi hiyo mshitakiwa ameweka mawakili wawili wa kumtetea. June mosi, Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa lilitangaza kumshikilia Prudence, mkazi wa Semtema-Kihesa kwa tuhuma za kuua mpenzi wake.
Prudence alidaiwa kuwa June mosi alimuua mwanafunzi mwenzake ambaye alikuwa mpenzi wake kwa kumnyonga.
Ilielezwa kabla ya tukio hilo, saa 12 jioni Petronila alifika nyumbani kwa mtuhumiwa pamoja na rafiki yake kwa lengo la kuchukua pesa yake Sh5,000 aliyokuwa akimdai mpenzi wake huyo.