Waziri: Majaribio dawa ya Ukimwi hayakuwa halali - 3

0

 



Jana katika sehamu ya pili ya habari inayohusu Watanzania waliofanyiwa majaribio ya dawa ya kutibu ugonjwa wa Ukimwi, Virodene, kati ya mwaka 2000 na 2001, tuliona jinsi waathirika hao walivyopata taarifa na kushawishiwa kushiriki katika majaribio hayo.

Waathirika hao ambao baadaye walifungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu kupinga miili yao kutumika kwa majaribio hayo, walidai kuwa madaktari kutoka Jeshi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi ndio waliowashawishi kujiunga na majaribio hayo.

Walidai pia wahudmu wa vituo vya afya vya mashirika yasiyo ya kiserikali walikokuwa wakipatiwa huduma waliwashawishi kujiorodheshe kwa ajili ya majaribio hayo.

Walieleza pia utaratibu na vigezo vya kushiriki na jinsi walivyoaminishwa kuwa majaribio ya dawa hiyo yaliyoendeshwa na kampuni ya Virodene Pharmaceutical Holdings Ltd ya Afrika Kusini ilikwishaonyesha mafanikio makubwa katika nchini mablimbali na kwamba wao na wenza wao watatibiwa bure pindi utafiti wa dawa hiyo utakapokamilika na baada ya hapo walitakiwa kurudi nyumbani kusubiri matokeo ya majaribio. Nini kilitokea baada ya majaribio hayo kukamilika? Endelea…

Baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani, waathirika hao waliendelea kusubiri kupata mrejesho chanya kwa kuwa waliahidiwa endapo dawa hiyo ingeonesha mafanikio, wao pamoja na wenzi wao wangetibiwa bure.

Hata hivyo, siku, majuma, miezi na hata miaka ilipita bila kupata mrejesho wowote wa hatima ya majaribio yaliyofanyika kwa kutumia miili yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable