Mazito yaibuka mama na bintize wakizikwa Dar

0
aziko pic

Waombolezaji wakiwa katika makaburi ya Kondo-Ununio wakati wa mazishi ya Emily Mutaboyerwa na mabinti zake Daniela na Damita, yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Picha na Sunday George

Dar es Salaam. Wakati mwili wa Emily Mutaboyerwa na wanawe wawili ikizikwa Juni 14, 2021 jijini Dar es Salaam, mambo mazito yameibuka baada ya zoezi la kuagwa kushindikana kutokana na miili hiyo kuharibika kwa majeraha.

Emily na wanane Daniela na Damita waliuawa Juni 9 mwaka huu na inadaiwa Shadrack Kapanga (34), aliyekuwa mlinzi katika nyumba waliokuwa wanaishi eneo la Masaki ndio alihusika.

Akizungumza jana wakati wa misa ya kuaga miili hiyo iliyofajika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Martha Mikocheni, msemaji wa familia, Alphonce Mutaboyerwa alisema ni vigumu kuzungumza na kwa wale walioiona miili hiyo siku ya tukio ni vigumu kujua kama ukatili huo ulifanywa na binadamu.

Alphonce ambaye pia ni shemeji wa marehemu, alisema ni vigumu kufungua majeneza hayo na kutoa heshima za mwisho, kwani hata wale waliokuwepo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakati miili ikifanyiwa uchunguzi watakubaliana na kauli hiyo.

“Maandiko yanasema shukuruni kwa kila jambo, hatuwezi kuzungumza mengi kwa kuwa upelelezi unaendelea, na yule aliyetenda anahadithia kama kilichotokea ni sinema.

“Hawa watoto walikosa nini? tuombe Mungu tupate nguvu ya kuzika salama na tunamoishi na watu tujifunze kuwasoma na kuwafahamu na kumchunguza kwa undani,” alisema Alphonce.

Akisoma wasifu wa marehemu, Judith Odunga alisema Emily alizaliwa Julai 13,1972, Dar es Salaam akiwa mtoto wa kwanza kati ya wawili wa mzee Ezekieli.

“Julai mwaka 2000 alifunga ndoa na Joseph Mutaboyerwa na kubahatika kupata watoto wawili; Daniela (15) na Damita (13) waliokuwa wanasoma shule ya Haven of Peace Academy (HOPAC),” alisema Odunga.

Katika misa ilyoongozwa na Paroko Msaidizi, Dominic Somola aliwataka waumini kuomba huruma ya Mungu kwa ajili ya marehemu waliotangulia pamoja na ulimwengu mzima.

“Tumekusanyika tukiwa tumekutana katika hisia za majonzi, somo la faraja ni tumaini ambalo litaweza kuhuwisha mioyo yetu.

“Huduma na utumishi aliokuwa nao Emily ni uzao aliouruhusu Mungu na wema aliokuwa nao hadi anafikwa na mauti, Mungu apokee huduma na utumishi aliokuwa nao ambao ametuachia,” alisema Paroko Somola.


Mkurugenzi shule waliyosoma watoto

Mkurugenzi wa shule ya HOPAC, Ricky Lewis alisema uongozi wa shule umepokea kwa masikitiko na mshtuko mkubwa vifo vya wanafunzi hao, kwani walikuwa na ndoto ambazo zimeshindwa kutimia.

Alisema Damita alikuwa mwanafunzi mchangamfu, mcheshi na mcha Mungu licha ya udogo wake, uongozi wa shule pamoja na wanafunzi wenzake wamepokea vifo hivyo kwa mshtuko.


Alivyoishi na wenzake

Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria mazishi hayo yaliyofanyika makaburi ya Kondo- Ununio walisema wanafunzi hao walikuwa wacheshi na wakarimu.

“Damita na Daniela walikuwa wanafunzi wakarimu na walikuwa na marafiki wengi waliojumuika kwenye shughuli mbalimbali zilizokuwa zinafanyika shuleni kila siku,” alisema Abdul Kharim.


Walichokisema Polisi

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, wanamshikilia Kapanga ambaye alikamatwa Juni 11, jioni maeneo ya Magomeni akiwa kwenye harakati za kutoroka akiwa na baadhi ya vitu alivyodaiwa kuiba baada ya kufanya tukio hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable