Staa wa muziki nchini Baraka the Prince hatimaye leo amethibitisha kuwa ameachana na mrembo Naj ambaye walikuwa wapenzi kwa miaka kadhaa. Barakah ameeleza hayo kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM.
Akifunguka hilo Baraka the Princeamesema ni miezi 8 imepita tangu waachane. Kwa sasa ushkaji ndio unawaweka pamoja.
Sanjali na hilo, Baraka the Prince ana wimbo wake mpya uitwao #Yanachosha ukiwa tayari na video yake. Gusa link kwenye bio ya Baraka the Prince kuitazama video ya wimbo huo.