Rais Biden anafanya mazungumzo na kundi la magavana kutoka majimbo manane ya Magharibi mwa Marekani
Rais wa Marekani Joe Biden anafanya mazungumzo Jumatano na kundi la magavana kutoka majimbo manane ya Magharibi mwa Marekani kuhusu kujiandaa na moto wa nyikani wakati eneo lote hilo linapambana na ukame.
Biden na maafisa wengine wa utawala watazungumza kutokea Ikulu na magavana kwa njia ya video.
Msemaji wa White House Jen Psaki aliwaambia waandishi wa habari wiki iliyopita mkutano huo utazingatia jinsi serikali kuu inavyoweza kuboresha matayarisho ya kupambana na moto wa nyikani na juhudi za kujibu, kulinda usalama wa umma, na kutoa msaada kwa watu wakati wa mahitaji ya haraka.
Tags
bongo habari