CCM: Kama kiongozi hujafanya chochote isahau nafasi yako mwakani

0


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimewatahadharisha viongozi wa Chama hicho walioshindwa kufanya kazi kwa ufasaha kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita ndani ya Chama katika uongozi wao na kuwataka kusahau nafasi hizo katika uchaguzi ujao wa mwaka 2022.

Hayo yamebainishwa na katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe Amina Imbo wakati akitoa salamu za Chama hicho katika baraza la jumuiya ya wazazi mkoa lililofanyika katika ukumbi wa ofisi za Chama hicho zilizopo Mji mwema halmashauri ya mji wa Njombe.

“Tunaelekea kwenye uchaguzi mwakani,kama kiongozi hujaweka alama katika eneo lako,haujafanya kazi kwa ufasaha katika jumuiya na Chama,ujue umejipoteza mwenyewe hatutaweza kukupa tena miaka miatano wakati tuliyokupa hukufanya chochote wala kubuni chochote,hiyo haikubaliki katika Chama cha Mpainduzi na Jumuiya zake”alisema Amina Imbo

Aidha ametoa wito kwa jumuiya ya wazazi kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu kwa kuwa jumuiya hiyo ndiyo iliyobeba jumuiya zingine katika Chama.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Njombe Jassel Mwamwala katika salamu zake ametoa wito kwa viongozi na wanachama wa Chama hicho kuongeza kasi ya kutafuta wanachama wapya ili kuimarisha zaidi Chama hicho.

“Tumetangaza 1 mara 3 kwa kila mwanachama maana yake kila mwanachama kwenye jumuiya utuletee wanachama watatu ili Chama kiwe na Nguvu,huwezi kuwa na Chama kama huna wanachama.Na jambo jingine tunahitaji ada,ni lazima tulipe ada na viongozi tuwe wa mfano”alisema Mwamwala

Baadhi ya wajumbe wa katika baraza hilo akiwemo katibu wa jumuiya ya wazazi mkoa Bi, Agatha Lubuva na mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Njombe Kasanga Makweta wamesema viongozi wataendelea kushiriakiana pamoja na kuhamasisha wanachama kulipa ada ya uanachama zoezi litakaloambatana na uuongezaji wanachama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable