Makete:Moto wateketeza bweni shule ye sekondari Ikuwo


Na Amiri Kilagalila,Njombe 

Bweni la wasichana shule ya Sekondari Ikuwo wilayani Makete mkoani Njombe limeteketea kwa Moto huku ikisadikika chanzo chake kuwa ni hitilafu ya Umeme au mkaa ulioanzia Chumba cha Matron (Mlezi wa wanafunzi)

Moto huo ulioanza asubuhi Leo majira ya saa moja umeteketeza vitanda vitanda, magodoro, Nguo za Wanafunzi pamoja na Vifaa vyao  huku Wanafunzi wote. Wakiwa salama

Jumla ya thamani ya vitu vilivyoteketea bado haijajulikana huku tathmini ikiendelea kufanyika

Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya, Mkurugenzi mtendaji wilaya na wataalamu mbalimbali wamefika kuangalia mali zilizoteketea kwa Moto huo uliotokea

Post a Comment

Previous Post Next Post