Chama cha Ukombozi cha Kitaifa (FLN) chashinda uchaguzi mkuu nchini Algeria

0


Chama cha Ukombozi cha Kitaifa (FLN) kilikuwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 12 Juni nchini Algeria kwa kupata jumla ya viti 105.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (ANIE) Mohammad Sharfi, ambaye alisimamia uchaguzi nchini Algeria, alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba FLN ilipata viti 105, vinavyolingana na asilimia 25.79 ya bunge lenye viti 407, na kuwa mshindi wa uchaguzi.

Akibainisha kuwa vyama vya kujitegemea vilishinda viti 78 sawa asilimia 19.16, chama cha Harakati ya Jamii ya Amani chenye mwelekeo wa Kiislamu kilishinda viti 64 sawa na asilimia 15.72, na chama cha Democratic National Unity (RND) kilishinda viti 57 sawa na asilimia 14, Sharfi pia alisema kuwa Mustakbel Front kilishinda viti 48 na Harakati ya Ujenzi wa Kitaifa kilishinda viti 40.

Sharfi alieleza kuwa  viti 15 vilivyobaki viligawanywa moja kwa moja kati ya vyama vingine vidogo,.

Akibainisha kuwa FLN ilishinda viti vyote 13 katika jimbo la Celfa, na viti vyote 8 katika jimbo la Musteganim vilichukuliwa na Harakati ya Ujenzi wa Kitaifa, Sharfi alisema kwamba bunge kubwa litaundwa na vijana, wanafunzi wa vyuo vikuu na wanawake.

Sharfi pia alifahamisha kuwa mfumo mpya wa orodha iliyo wazi unaruhusu kanuni kwa njia ya uwakilishi wa watu bungeni.

Asilimia 30.2 tu ya wapiga kura milioni 24 waliojiandikisha walijitokeza kupiga kura zao katika uchaguzi wa Juni 12, ambapo upinzani ulitoa wito wa kususia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable