Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema umoja huo unahitaji kuisukuma nyuma, kuibana na kuishirikisha Urusi, wakati viongozi wa Urusi na Marekani wakikutana jijini Geneva. Akizunumgza wakati akiwasilisha ripoti mpya inayoeleza mkakati wa kujenga uhusiano imara na Urusi, Borrell amesema wanaamini kwamba kuwa na ushirikiano mpya, na kutambua uwezo kamili wa ushirikiano wa karibu na Urusi ni matarijio yasiyowezekana kwa urahisi na kwa hiyo Umoja wa Ulaya, unahitaji kuwa mkweli na kujiandaa kwa mtikisiko zaidi wa mahusiano yao na Urusi. Mahusiano kati ya Urusi na Umoja wa Ulaya wenye nchi wanachama 27 yamefikiwa kiwango cha chini baada ya umoja huo kuiwekea Moscow vikwazo kuhusiana na kukamatwa kwa mkosoaji wa ikulu ya Kremlin Alexei Navalny na hatua ya mamlaka za Urusi kujibu kwa kuwalenga maafisa wa Umoja wa Ulaya. Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatafuta msimamo wa pamoja wa kushirikiana na jirani yake huyo wa mashariki licha ya mgawanyiko miongoni wa mwanachama kuhusu jinsi ya kumkabili Rais wa Urusi Vladmir Putin.
