Stefan De Keersmaecker, mmoja wa wasemaji wa Jumuiya ya Ulaya (EU), alisema kuwa asilimia 55 ya idadi ya watu wazima tayari wamepewa dozi ya kwanza ya chanjo na asilimia 32 wamepewa dozi ya pili ya chanjo.
Keersmaecker alieleza kuwa kwa kuzingatia chanjo za sasa na uwasilishaji wa siku zijazo, lengo la kutoa chanjo kwa asilimia 70 ya watu wazima linaweza kufikiwa mwezi Julai, na kuongeza uwasilishaji wa dozi milioni 357 na laki 7 kwa EU.
Keersmaecker alitangaza kuwa dozi milioni 310 na laki 7 kati yao tayari zimewasilishwa nchini na kusajiliwa.
Keersmaecker aliongezea kusema kuwa kulingana na data ya wiki iliyopita, zaidi ya dozi milioni 25 za chanjo zimekuwa zikitolewa kwa wiki, na kwamba wanaendelea kufanya kazi ili kumaliza tofauti kati ya nchi wanachama.
Wakala wa Dawa za Ulaya (EMA) hadi sasa wameidhinisha utumiaji wa chanjo 4 katika nchi za EU.
Hizi ni pamoja na chanjo zinazozalishwa na BioNTech-Pfizer, Moderna, AstraZeneca na Johnson & Johnson.