Hospitali ya Afghanistan yaungua baada ya shambulio la roketi

0


Maafisa wa serikali wa Afghanistan wamesema wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wa kundi la Taliban wamefanya shambulizi la roketi ndani ya hospitali nchini humo na kusababisha uharibifu mkubwa ikiwemo kuharibu chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 na vifaa vyengine muhimu.Maafisa hao hata hivyo wamesema hakukuwa na ripoti za majeruhi.Msemaji wa kundi la Taliban Zabihullah Mujahid amekanusha kuhusika na shambulio hilo la hospitali lililotokea katika mkoa wa mashariki wa Kunar.Mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi yameongezeka katika wiki za hivi karibuni, huku waasi hao wakiendelea kuchukua udhibiti wa sehemu muhimu wakati vikosi vya jumuiya ya kujihamu ya NATO vikijiandaa kuondoka kabisa nchini humo.Kaskazini mwa Afghanistan, kundi la Taliban liliuteka mji wa Shir Khan Bandar, bandari kavu iliyoko mpakani na Tajikistan na kuwafanya wafanyikazi wa forodha na baadhi ya vikosi vya usalama kukimbilia usalama wao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable