Mbappe na Ronaldo kukutana katika mechi itakayoamua mustakabali wa timu ya taifa ya Ureno
Timu ya taifa ya Ufaransa inaingia uwanjani hii leo kukabiliana na Ureno katika mechi ambayo itawakutanisha nyota Kylian Mbappe na Cristiano Ronaldo kwenye mechi ya kundi F.Mechi hiyo inatajwa kuwa muhimu kwani huenda ikaamua mustakabali wa timu ya taifa ya Ureno katika michuano ya Euro.Ufaransa inaongoza kundi F ikiwa na alama nne, alama moja mbele ya Ujerumani iliyoko katika nafasi ya pili, wakati mabingwa watetezi Ureno ikiwa katika nafasi ya tatu na Hungary inashikilia mkia ikiwa na alama moja.Na katika mechi nyengine zitakazotifua vumbi hii leo, Slovakia itacheza na Uhispania wakati Sweden ikiwa katika uwanja wa Saint Petersburg kuchuana na Poland.

