Korea Kaskazini yatoa msaada wa dola 300,000 kwa Myanmar

0



Korea Kaskazini imetoa dola laki tatu kwa mpango wa msaada wa kibinadamu unaoongozwa na Umoja wa Mataifa kwaajili ya myanmar, ikiwa ni mchango wake wa kwanza kwa mataifa mengine tangu mwaka 2005, kwa mujibu wa data za Umoja wa Mataifa. Data kutoka kitengo cha ufuatiliaji wa huduma za kifedha cha ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kiutu OCHA, zinaonesha kuwa Korea Kaskazini ilitoa mchango huo Mei 24 kwa Mfuko wa Kiutu wa Myanmar. Mfuko huo uliomba kiasi cha dola milioni 276 kuisadia Myanmar, ambako mamia ya watu wamekufa tangu jeshi lilipoipindua serikali iliyochaguliwa iliyoongozwa na Aung San Suu Kyi mnamo Februari mosi, na kuanzisha ukandamizaji dhidi ya waandamanaji wanaopigania demokrasia, na kuongezea kwenye mapambano ya nchi hiyo dhidi ya janga la virusi vya corona.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable