Migogoro imeongezeka tangu kuanza janga la COVID 19

0





Viwango vya migogoro duniani vimeripotiwa kuongezeka tangu kuanza kwa janga la COVID 19, hii ikiwa ni kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya Faharasi ya Amani ya Dunia, iliyochapishwa hii leo na taasisi ya uchumi na amani. Ripoti hiyo inayotathmini hali katika mwaka wa 2020, inaonesha kuwa migogoro imeongezeka kwa mara ya tisa katika muda wa miaka 12. Muanzilishi wa taasisi hiyo Steve Killelea amesema janga la corona ndilo linalopaswa kulaumiwa kwa ongezeko hilo. Ameongeza kuwa licha ya viwango jumla vya mizozo na ugaidi kupungua mwaka 2020, ukosefu wa utulivu wa kisiasa na maandamano ya vurugu viliongezeka. Ripoti hiyo imesema athari za kiuchumi zinazotokana na janga la corona zitasababisha mashaka zaidi, hasa kwa mataifa ambayo tayari yalikuwa yanakabiliwa na hali ngumu kabla ya janga la corona.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable