Utata unaozunguka hatua ya serikali ya kaunti ya Nairobi kuipatia barabara moja jijini humo ya jina la katibu wa muungano wa wafanyakazi humu nchini Farncis Atwoli unaendelea kufukuta.
Katika hatua ya hivi punde bango hilo lililowekwa katika barabara ya Dik Dik na kupewa jina la Farncis Atwoli limechomwa moto.
Tangu lilipobomolewa mara y akwanza mwishoni mwa mwezi Mei lilimekuwa likipewa ulinzi.
Atwoli alikerwa na waliotekeleza shughuli hiyo na kutaka polisi kuazisha uchunguzi mara moja ili wawajibishwe kisheria.
Wanaopinga kuwekwa kwa bango hilo wamekuwa wakitumia mtandao wa Twitter kuelezea malalamiko yao huku baadhi wakisema ni ukiukaji wa sheria.
