Maelfu ya watu wamelazimika kutoroka makwao Image caption: Maelfu ya watu wamelazimika kutoroka makwao Mamlaka nchini Msumbiji zimesema kuwa zaidi ya raia 9,600 wa Msumbiji wanaokimbia vurugu kaskazini mwa Jimbo la Cabo Delgado "wamerudishwa kwa nguvu" kutoka Tanzania tangu Januari 2021, Diario de Noticias gazeti binafsi nchini humo limeripoti.
Kulingana na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa karibu watu 900 "walisukumwa kw alazima " kuvuka mpaka kati ya tarehe 7 na 9 Juni.
Ripoti hiyo inakuja saa chache baada ya manusura walionukuliwa na tovuti inayomilikiwa na watu binafsi O Pais, kufichua kwamba mji wa Palma kaskazini mwa Msumbiji, ulibaki ukikaliwa na wanamgambo, ambao wanachama wao wanaendelea "kuchoma nyumba, kuua na kuteka nyara watu".
Mashambulio makubwa ya hivi karibuni ya kundi hilo dhidi ya mji wa Palma mnamo 24 Machi, yaliwahamisha zaidi ya watu 70,000, na kuongeza idadi ya watu waliohamishwa kutokana na ghasia kaskazini mwa Msumbiji hadi karibu 800,000.