Homebongo habariLebanon yazidi kuporomoka kiuchumi kufuatia mvutano wa kisiasa Lebanon yazidi kuporomoka kiuchumi kufuatia mvutano wa kisiasa 0 ben June 14, 2021 Sarafu ya pauni ya Lebanon imeporomoka kwa mara nyingine wakati nchi hiyo ya mashariki ya kati ikishuhudia kuongezeka mgogoro wa kiuchumi na kisiasa. Mgogoro huo hauna ishara ya kumalizika hivi karibuni. Sarafu ya nchi hiyo imepoteza thamani kwa zaidi ya asilimia 90 tangu mwezi Oktoba mwaka 2019 baada ya kuzuka maandamano makubwa ya kuipinga serikali. Mfumko wa bei umeongezeka na bei za bidhaa za msingi zimepanda kwa kiwango kikubwa katika nchi hiyo ambayo asilimia 80 ya bidhaa zake za msingi zinaagizwa kutoka nje. Kuporomoka kwa sarafu mara hii kumekuja wakati nchi hiyo ndogo ikiwa inashuhudia ukosefu mkubwa wa bidhaa muhimu kama mafuta na dawa. Mvutano wa kisiasa kati ya rais Michel Aoun na waziri mkuu mteule Saad Hariri umechelewesha uundwaji serikali mpya. Hariri alichaguliwa mwezi Oktoba mwaka jana. Tags bongo habari Newer Older