Homebongo habariVisa vya maambukizi ya Corona vyapungua Ujerumani Visa vya maambukizi ya Corona vyapungua Ujerumani 0 ben June 14, 2021 Waziri wa afya nchini Ujerumani Jens Spahn amesema kupitia tamko lake lililochapishwa kwenye vyombo vya habari nchini humo leo kwamba kushuka kwa viwango vya maambukizi nchini humo kunamaanisha kwamba hatua ya lazima ya kuvaa barakoa kwenye maeneo ya umma huenda ikaondolewa. Ameliambia shirika la habari la Funke kwamba Ujerumani inapaswa kuchukua uamuzi huo hatua kwa hatua kwa kuzingatia maeneo ambayo visa vya maambukizi vimepungua. Katika maeneo ya Ujerumani ambako viwango vya maambukizi viko chini na idadi kubwa ya watu wamepata chanjo, amri ya uvaaji barakoa inaweza pia kuondolewa katika maeneo ya ndani, lakini amesisitiza kwamba barakoa zinapaswa kuendelea kuvaliwa katika baadhi ya nyakati ikiwa kuna wasiwasi kwa mfano watu wanaposafiri au kwenye mikusanyiko ya maeneo ya ndani. Hata hivyo walimu wameipinga mara moja hatua hiyo ya kuondoa barakoa.Rais wa chama cha walimu nchini Heinz Peter Meidinger ametowa mwito wa kuchukuliwa tahadhari kubwa. Tags bongo habari Newer Older