Homebongo habariWanasiasa watano wa upinzani wakamatwa Nicaragua Wanasiasa watano wa upinzani wakamatwa Nicaragua 0 ben June 14, 2021 Wanasiasa watano wa upinzani nchini Nicaragua wamekamatwa ikiwa ni miezi mitano kabla ya uchaguzi wa rais. Wanasiasa hao ambao wengi ni wanachama wa chama cha Union Democratica Renovadora-UNAMOS walikamatwa mwishoni mwa juma kwa mujibu wa gazeti linaloikosoa serikali La Prensa. Waliokamtwa ni pamoja na mgombea urais wa chama cha upinzani cha UNAMOS Suyen Barahona, makamu wa rais na jenerali mstaafu Hugo Torres, pamoja na mpiganaji wa zamani wa vita vya msituni Dora Maria Tllez na Ana Margarita. Wanasiasa hao wamekamatwa kwa madai ya kupanga njama za kufanya matukio ya kigaidi kwa ufadhili wa nchi za kigeni zenye nguvu. Wagombea urais Arturo Cruz, Felix Maradiaga na Juan Chamorro nao pia wamekamatwa kwa kuhisishwa na madai hayo hayo. Wakosoaji wanaituhumu serikali ya rais Daniel Ortega aliyeko madarakani tangu mwanzoni mwa 2007 kutaka kuubana upinzani na kuzuia uchaguzi huru na wa haki. Tags bongo habari Newer Older