Homebongo habariAung San Suu Kyi afikishwa mahakamani Aung San Suu Kyi afikishwa mahakamani 0 ben June 14, 2021 Kiongozi wa Myanmar aliyeondolewa kwa nguvu madarakani na jeshi, Aung San Suu Kyi leo amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka ambayo waangalizi wamekuwa wakikosoa kwamba ni juhudi za utawala wa kijeshi za kutaka kumdhoofisha kisiasa baada ya kumuondowa kwa njia zisizokuwa halali. Suu Kyi anashtakiwa kwa madai ya kuwanunulia walinzi wake kinyume cha sheria simu za upepo, na kutumia simu hizo bila kibali pamoja na kusambaza taarifa ambazo zingeweza kusababisha taharuki na machafuko nchini humo. Aidha anatuhumiwa kuhusika na makosa mawili ya kukiuka sheria za usimamizi wa majanga ya asili ambapo kwa mujibu wa wakili wake anadaiwa alikiuka vizuizi vya kukabiliana na janga la virusi vya Corona wakati wa kampeini ya uchaguzi mwaka 2020. Hatua ya kushtakiwa kiongozi huyo wa kiraia inasababisha changamoto kubwa kwake na chama chake cha National League for Democracy NLD tangu yalipofanyika mapinduzi ya kijeshi yaliyomzuia kiongozi huyo na chama chake kuingia madarakani kuongoza muhila wa pili wa miaka mitano, baada ya kupata ushindi mkubwa. Shirika la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch limeyaita madai yanayosikilizwa katika kesi hiyo kwenye mahakama maalum mjini Naypitaw, hayana maana na yaliyochochewa kisiasa yenye lengo la kuufuta ushindi wa Suu Kyi na chama chake na kumzuia asigombee tena uongozi nchini humo. Tags bongo habari Newer Older