Homebongo habariChina yakasirishwa na azimio la viongozi wa G7 China yakasirishwa na azimio la viongozi wa G7 0 ben June 14, 2021 China imelaani taarifa ya pamoja iliyotolewa na kundi la nchi tajiri za G7 mjini London ambayo imeikosoa vikali Beijing kuhusu masuala kadhaa. China imeiita hatua ya G7 kwamba ni uingiliaji masuala ya ndani ya nchi yake na kulitaka kundi hilo likome kuiponda nchi yake. Jana Jumapili viongozi wa G7 waliishambulia China kuhusu suala la haki za binadamu katika jimbo la Xinjiang linalokaliwa na jamii ya waislamu na kuitolea mwito Hong Kong kuimarisha mamlaka yake ya ndani na kusisitiza juu ya umuhimu wa amani na uthabiti katika eneo zima la Taiwan. Ubalozi wa China mjini London umesema umekasirishwa sana na azimio la G7 na hasa kutokana na kutajwa kwa suala la Xinjiang, Hong Kong na Taiwan kwa njia ya upotoshaji ukweli na kuonesha nia ovu ya nchi chache kama Marekani. Ubalozi huo umesema China ni nchi inayopenda amani inayohimiza ushirikiano lakini pia ina mipaka yake ikiwemo kutotaka kuingiliwa masuala yake ya ndani. Tags bongo habari Newer Older