Homebongo habariRais Erdogan ataraji kumaliza tafauti zake na Biden Rais Erdogan ataraji kumaliza tafauti zake na Biden 0 ben June 14, 2021 Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kwamba yeye pamoja na rais wa Marekani Joe Biden wanabidi kutumia mkutano wa leo Jumatatu wa jumuiya ya kujihami ya NATO kuondowa tafauti zilizopo ikiwemo mvutano mbaya kuhusu suala la Uturuki kununua makombora ya Urusi chapa S-400. Erdogan ametowa kauli hiyo kabla ya kwenda Brussels ambako leo atashiriki mkutano wa kilele wa NATO. Amesema anatarajia Marekani haitochukua mwelekeo wa kuweka masharti wakati atakapokaa na Biden kwa mara ya kwanza katika kikao cha ana kwa ana tangu ulipofanyika uchaguzi wa Marekani mwaka jana. Kadhalika Erdogan amesema kwamba atalizusha suala la hatua ya Washington kuyatambua mauaji ya halaiki ya mwaka 1915 ya Warmenia chini ya utawala wa Ottoman kama mauaji ya kimbari. Uturuki ilikasirishwa sana na hatua hiyo pamoja na hatua ya Marekani kuiondowa Uturuki katika mpango wa kuiuzia ndege za kivita aina ya F-35. Rais Erdogan ambaye amekuwa akitegemea uhusiano binafsi wa karibu na mtangulizi wa Biden, Donald Trump kuimaliza mivutano ya zamani, amejikuta kwenye hali ngumu ya kukosolewa na kutengwa na utawala wa sasa wa Marekani. Tags bongo habari Newer Older