Homebongo habariRais Joe Biden yuko Brussels kushiriki mkutano wa kilele wa NATO Rais Joe Biden yuko Brussels kushiriki mkutano wa kilele wa NATO 0 ben June 14, 2021 Rais wa Marekani Joe Biden leo atashiriki mkutano wa kilele wa jumuiya kujihami ya NATO ambapo analenga kushauriana na washirika wake wa Ulaya kuhusu juhudi za kukabiliana na vitendo vya uchokozi vinavyofanywa na China na Urusi wakati pia akionesha kujitolea kwa Marekani katika muungano huo wenye wanachama 30 uliokuwa ukishambuliwa mara kwa mara na mtangulizi wake Donald Trump. Mkutano huo wa kilele wa leo unakuja wakati Biden akijaribu kukusanya washirika kwa ajili ya kupata ushirikiano mkubwa katika kuzikabili China na Urusi. Marekani ina wasiwasi na vitendo vya nchi hizo mbili kuelekea masuala ya uchumi na usalama wa nchi yake ambayo ndiyo masuala yake muhimu katika sera yake ya nje. Katika mkutano huo Biden anatarajiwa kusisitiza juu ya kujitolea kwa nchi yake katika muungano huo kwa kuzingatia sheria namba 5 ya muungano huo ambayo inaweka wazi kwamba kushambuliwa kwa nchi moja mwanachama ni sawa na kushambuliwa jumuiya nzima, na hatua hiyo inabidi ijibiwe na jumuiya yote. Tags bongo habari Newer Older