Marekani yaweka vikwazo dhidi ya mtandao wa Yemen unaodaiwa kushirikiana na Iran

0



Marekani ineuwekea vikwazo mtandao wa nchini Yemen unaodaiwa kushirikiana na jeshi la mapinduzi la Iran katika kuwapelekea mamilioni ya dola waasi wa Houthi kinyume cha sheria. Wakati huo huo, utawala wa Rais Biden umetangaza kuwaondolea vikwazo wakurugenzi watatu na kampuni moja. Marekani imesema kampuni hiyo na wakurugenzi hao, hapo awali walishiriki katika mauzo ya mafuta yaliyopigwa marufuku. Marekani imeeleza kuwa imebainisha mabadiliko katika hali na nyendo za wakurugenzi na kampuni hiyo ya Iran. Hatua hiyo imechukuliwa wakati utawala wa Rais Biden unajaribu kuwashinikiza waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran washiriki kwenye mazungumzo ya kumaliza vita vya nchini Yemen na wakati huo huo ambapo utawala wa Biden unaendelea na mazungumzo juu ya Marekani kurejea kwenye mkataba wa nyuklia na Iran.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable