Mawaziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani wajadili chuki dhidi ya Mayahudi, wanawake na waandishi

0


Mawaziri wa mambo ya ndani wa majimbo ya nchini Ujerumani wamekubaliana kuongeza mapambano dhidi ya visa vya chuki dhidi ya Mayahudi na unyanyasaji dhidi wanawake. Aidha wamekubaliana kuwalinda waandishi wa habari dhidi ya kushambuliwa wanapokuwa kwenye majukumu yao. Mawaziri hao wa majimbo 16 pamoja na wa shirikisho wamesema kuna haja ya kuvishughulikia viwango sawa na kanuni za kudhiti maandamano yanayowapinga Waisraeli yanayofanywa kwenye masinagogi ama kuyazuia kabisa na kuongeza viwango vya adhabu dhidi ya uhalifu wa chuki dhidi ya Mayahudi. Wakizungumzia unyanyasaji kwa wanawake, mawaziri hao wamesema kuvionea aibu hakutaleta suluhu na kukubaliana pia kwamba mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari hayana nafasi katika taifa lililo huru na la kidemokrasia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable