Mchungaji Bushiri: 'Mhubiri anayeweza kutembea angani'

Shepherd Bushiri

CHANZO CHA PICHA,SHEPHERD BUSHIRI/ FACEBOOK

Watu wanapiga makofi, wengine wanacheza densi na wengine wakirukaruka juu huku akiingia katika ukumbi , akiandamana na walinzi wake.

Hiyo ndio furaha ambapo baadhi ya waumini ambao walikuwa wamemsubiri kwa saa tano kumuona wanazirai.

Lakini kwanini wewe usizirai? Huyu ni mtu ambaye anasema kwamba ametibu watu wenye virusi vya HIV, amewafanya vipofu kuona, amebadilisha hali ya masikini na mara moja ameonekana akitembea angani.

Mtumishi wa Mungu kwa jina Bushiri amepitia mengi akilewa katika mji wa Mzuzu uliopo kaskazini mwa Malawi.

Siku hizi , anaweza kujaza viwanja vya michezo na maelfu ya waumini wake ni wafuasi ambao wako tayari kusafiri kote duniani ili kumuona akiongoza ibada yeye mwenyewe.

Uwanja wa FNB nchini Afrika kusini

CHANZO CHA PICHA,KANISA LA ECG

Ana wageni wa mara kwa mara kutoka Marekani, Uingereza na hata bara Asia - ambapo bendera zao hupepea ndani ya kanisa la Enlightened Christian Gathering, ECG .

Nakutana na mtu ambaye anajulikana kama 'Major One' katika kanisa lake katika mji mkuu wa Afrika Kusini Pretoria.

Tumekaribishwa katika kanisa lake , ambalo limezungushwa kamba nyekundu na zulia ambalo limewekwa na walinzi wake katika pande zote mbili.

'Kuwaponya walemavu'

Mhubiri huyo mwenye umri wa miaka 30 anajua kuhusu madai kwamba anaonekana kuwa bandia lakini hayo ni madai ambayo huyapuuzilia mbali.

''Kanisa langu sio la kila mtu, ni la wale walio na Imani'', ananiambia.

''Mimi ni mtumishi wa Mungu . Mungu huwaponya watu katika mikusanyiko yetu. Siku moja niliwambia madaktari hapa Pretoria walete wagonjwa wa virusi vya Ukimwi HIV - waliwapima ili kubaini iwapo ni wagonjwa , niliwaombea na wakabadilika na ugonjwa huo kuangamia''.

Je mtumishi Bushiri ni nani?

Mchungaji Bushiri

CHANZO CHA PICHA,ECG MINISTRIES

  • Ni muhubiri aliyezaliwa nchini Malawi na ambaye anamiliki makanisa kutoka Ghana hadi Afrika Kusini.
  • Alipigwa marufuku nchini Botswana kwa madai ya miujiza ya kutenegeza fedha.
  • Anadai kutibu HIV
  • Alionekana akitembea angani katika kanda ya video iliosambazwa katika mitandao ya kijamii
  • Anamiliki ndege binfasi

Nje ya kanisa hilo, wafuasi wake wanakubali. Wanaamini kwamba hana nguvu za utume pekee , lakini pia anawatibu wagonjwa na kuombea watu maisha mazuri.

''Miujiza na mafunzo ambayo mtumishi wetu hutufunza kila wiki ni nzuri,'' alisema Xolani Msibi mwenye umri wa miaka 24.

Anasema kwamba dada yake ambaye alikuwa na matatizo alitibiwa na mtumishi huyo bila kumuwekea mikono."

"Nimetatizika kupata kazi na nikaja hapa na nikapata kazi mbili wakati mmoja na nikalazimika kuchagua."

Wanaume na wanawake wanaodai kuwa na uwezo wa kufanya miujiza ni watu wa kawaida nchini Afrika Kusini ama hata barani Afrika - wanapatikana kutoka maeneo mbali mbali duniani. Wahubiri hao ni pamoja na kiongozi wa kanisa la Israel Benny Hinn, Grace Copeland na Muhubiri Rienhard Bonnke .

'Ustawi huwapatia msukumo wafuasi wangu'

Tukirudi kwa mtumishi Bushiri, kila siku ya Jumapili , takriban wafuasi 40,000 hukusanyika kusikiliza hotuba zake , kununua baadhi ya vitu vinavyouzwa ndani ya kanisa hilo kutoka mafuta ya miujiza , kalenda, bendi za mkono na taweli zenye nembo yake , Tisheti , kofia zote zikiwa na uso wake.

'Mafuta ya miujiza'

Mafuta haya ya miujiza yanauzwa nje ya kanisa hilo
Maelezo ya picha,

Mafuta haya ya miujiza yanauzwa nje ya kanisa hilo

Katika kipindi cha miaka kadhaa Bwana Bushiri amejilimbikizia utajiri. Na je anasemjje kwa wale wanaohoji jinsi anavyojipatia fedha zote hizo?

"Ni ubaguzi," anaiambia BBC .

Hakuna rekodi za utajiri wake zilizo tayari lakini anajulikana kuwa na hamu katika migodi kadhaa na anamiliki ndege nne za kibinafsi na baadhi ya hoteli , kupitia kampuni yake ya uwekezaji iliopo mjni Johannesburg Kijiji cha Sandton.

Haamini kwamba wahubiri wanapaswa kuishi maisha ya kadri

CHANZO CHA PICHA,KANISA LA ECG

Maelezo ya picha,

Haamini kwamba wahubiri wanapaswa kuishi maisha ya kadri

Maswali jinsi ya vile alivyojipatia utajiri wake hayaruhusiwi.

''Mafanikio yangu yanapaswa kuwapatia watu msukumo wa kuwa wafanyabiashara'' , anasema.

''Mimi ni mfanyabishara na hilo ni tofauti na utumishi . Ufanisi wangu unatokana na biashara za kibinfasi. Maswali kama hayo hayaulizwi na viongozi weupe wa makanisa lakini mwanamume wa Kiafrika anapofanikiwa , basi inakuwa tatizo'' .

Halafu anaongezea,'' inakuwaje tatizo ninapouza bidhaa kanisani mwangu kama vile Wakatoliki wanavyouza tasbihi huku makanisa ya Uingereza yakiuza biblia ? sio vizuri''.

Lakini je wazo la mtu wa Mungu kuishi Maisha ya kadri?

Je ana wsiwasi kwamba hivi ni vitu ambavyo wafuasi wake wachache watamiliki katika maisha yake.?

''Hapana! ufanisi wangu ni msukumo kwa wafuasi wangu - wanafikiria kwamba iwapo Mungu anaweza kuniwezesha basi hata pia anaweza kuwafanyia hata wao. Iwapo wanaamini kuna kitu chochote kibaya , wasingenifuata'', anaelezea.

Lakini ijapokuwa ni msukumuo kwa waumini wake , ufanisi wake wa muda mfupi umeonekana na wengi.

Ampokea vitisho kutoka kwa watu ambao wanamuona kama mshindani wao - na pia kuna wale walio na wasiwasi na watu wanaotumia fedha zao katika vibanda hivyo na wale walio katika makanisa kama hayo nchini humo kila Jumapili.

Je nani anaweza kushindana na mtumishi wa Mungu?

Kuna wasiwasi wa sheria za Afrika kusini kuhusu dini - kitu ambacho kilimruhusu bwana Bushiri kuimarisha kanisa lake kwa muda mfupi.

Ukivuka mpaka nchini Botswana , kanisa lake limefungwa kutokana na madai ya miujiza ya fedha hatua inayokiuka sheria za fedha nchini humo..

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post