Moto wazuka kusini mwa Israel kabla ya maandamano

0


Moto umezuka kwenye mashamba kusini mwa Israel leo kabla maandamano yaliyopangwa kufanywa na Mayahudi takriban 5,000 wenye misimamo mikali ya kizalendo katika eneo la mji mkongwe la Jerusalem. Idara ya zimamoto imesema matukio mawili ya moto yalisababishwa na mabofu mawili kutoka Ukanda wa Gaza. Video imeonesha maeneo makubwa ya nyasi zilizoungua. Makundi mawili makubwa ya Palestina, Fatah na Hamas, yameitisha siku ya ghadhabu. Maandamano hayo yameandaliwa na wafuasi wa waziri mkuu wa zamani, Benjamin Netanyahu. Maafisa 2,000 wa polisi wamepelekwa kupiga doria katika eneo hilo. Gazeti la Jerusalem Post limeripoti kuwa jeshi la Israel limetuma vikosi vya ziada Ukingo wa Magharibi ambako kuna uwezekano wa machafuko kuenea hadi eneo hilo. Katika mkutano na wajumbe wa vyombo vya usalama, Waziri wa Ulinzi wa Israel Benny Gantz amesisitiza juu ya umuhimu wa kuulinda usalama wa kila raia wa Israel, Mayahudi na Waarabu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable