Msumbiji ifanye mazungumzo na wanamgambo ili kumaliza uasi

0



Shirika la kimataifa linalofuatilia migogoro la ICG limeitolea mwito serikali ya Msumbiji kufanya mazungumzo na wanamgambo pamoja na kuunganisha nguvu za kijeshi katika kukabiliana na uasi unaozidi kuongezeka katika eneo la kaskazini lenye utajiri mkubwa wa gesi. Katika taarifa yake iliyoitoa hii leo, ICG imesema Msumbiji inahitajika kutatua masuala ya ndani yaliyosababisha wanamgambo kuanzisha vita ili kumaliza vurugu. Aidha shirika hilo limeitaka Msumbiji kutumia nguvu zake kwa busara na kukubali msaada wa kijeshi kutoka nje kwa uangalifu lakini wakati huohuo ikizingatia kukabiliana na uasi wa wanamgambo unaozidi kuenea na kuwalinda raia wanaokimbia makaazi yao. Wanamgambo wanaohusishwa na kundi linalojiita dola la Kiislamu IS, wamesababisha hofu na taharuki katika mkoa wa Capo Delgado tangu mwaka 2017 kwa kufanya uvamizi wa vijii na miji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

About Us

Light Speed Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are available Which is designed in User friendly to handle by Piki Developers. Simple and elegant themes for making it more comfortable